Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Mamama na watoto wake 10 wamehamia kwenye kambi ya wakimbizi Kenya mwaka 2022 baada ya ukame kusambaratisha mazao na mifugo yake Somalia
© UNHCR/Charity Nzomo

UNHCR imeomba dola milioni 137 kusaidia waliokimbia makazi yao Pembe ya Afrika

Ukanda wa Pembe ya Afrika ukiingia msimu wa sita bila mvua, ukimbizi wa ndani unazidi kushamiri kwa kuwa mamilioni ya watu kutoka Somalia, Ethiopia na Kenya wanaendela kuhaha katikati ya uhaba wa maji, njaa, ukosefu wa usalama na mizozo, amesema Olga Sarrado, msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR akizungumza na waandishi wa habari hii leo huko Geneva, Uswisi. 

Walinda amani wanahamasisha jamii kufanya shughuli za maendeleo kwa ajili ya nchi yao ya Jamhuri ya Afrika ya Kati
© MINUSCA

Walinda amani wa UN kutoka Tanzania wametufundisha kutumia majembe – Wakulima CAR 

Wananchi wa Kijiji cha Difolo katika viunga vya mji wa Berberati mkoa wa Mambéré-Kadéï nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR wamewashukuru walinda amani wa kikosi cha 6 kutoka Tanzania kinachohudumu chini ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo (MINUSCA) baada ya wanalinda amani hao kuwafundisha wananchi hao kulima kwa kutumia jembe la mkono badala ya kulima kwa kutumia panga.  

Kampeni ya chanjo ya kipindupindu imezinduliwa katika wilaya ya Caia jimboni Sofala nchini Msumbiji
© Sofala District Health Directorate/Zainabo

Kampeni ya chanjo ya kipundupindu Msumbiji yalenga watu 720,000: WHO

Shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO limesema Msumbiji leo imeanza kampeni ya chanjo ya kipindupindu inayolenga takriban watu 720,000 katika wilaya nane huku nchi hiyo ikichukua hatua za kudhibiti kusambaa kwa mlipuko huo ambapo hadi sasa wagonjwa 5260 na vifo 37 vimerekodiwa tangu kuzuka Septemba 2022. 

Familia ikiwa imekaa kwenye makazi ya wakimbizi wa ndani mjini Aden Yemen
© UNHCR/Ahmed Al-Mayadeen

Dola bilioni 4.3 zahitajika kwa ajili ya mahitaji ya kibinadamu Yemen 2023:UN

Wahisani wa kimataifa wanakutana leo mjini Geneva Uswis kwa ajili kutanabaisha kuhusu zahma ya kibinadamu inayoendelea nchini Yemen na kuchangisha fedha za kufadhili operesheni za kibinadamu nchini humo. Mkutano huo wa ngazi ya juu wa kuchangisha fedha kwa ajili ya Yemen umeandaliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na serikali za Sweden na Uswis. 

Sauti
2'40"