Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Octavia akiwa na tabasamu na hii yote ni baada ya kurejea shuleni kupitia programu ya UNICEF.
UNICEF Kenya/2023/Translieu

Elimu ni haki ya msingi ya kila mtoto ndio maana tunachukua hatua Kenya kuhakikisha hilo- UNICEFF

Elimu ni moja ya nyenzo zenye nguvu zaidi za kuleta mabadiliko kwa watu binafsi na jamii na ndio maana katika miongo miwili iliyopita, serikali ya Kenya imefanya mageuzi mengi ili elimu ya msingi iwe bure na ya lazima kwa watoto wote walio katika umri wa kwenda shule. 

Hata hivyo, watoto wengi bado hawako shuleni kutokana na umaskini, miundombinu duni, kutelekezwa na wazazi na matatizo ya kiafya hasa katika maeneo masikini. Sasa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limeamua kuingilia kati kwa kushirikiana na wadau kusaidia.

Sauti
2'53"
Vijana wawili waathirika wa usafirishaji haramu wa binadamu, ambao waliokolewa kutoka kambi ya wakimbizi ya Dzaleka, wanapokea msaada katika makazi nchini Malawi.
© UNODC

Hakuna mtu anayepaswa kununuliwa, kuuzwa au kufanywa mtumwa – Katibu Mkuu UN

Usafirishaji haramu wa binadamu ni ukiukwaji mkubwa wa haki za kimsingi za binadamu na uhuru. Inawinda watu wasio na ulinzi na hustawi wakati wa migogoro na ukosefu wa utulivu. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres katika ujumbe wake kuhusu Siku ya Kimataifa dhidi ya Usafirishaji Haramu wa Binadamu ambayo huadhimishwa kila tarehe 30 Julai.