Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Wafanyakazi wengi nchini Marekani wamenaswa katika mtego wa umaskini kutokana na mishahara duni; kwa mujibu wa mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa.
© Unsplash/Tobias

Amazon, DoorDash na Walmart walaumiwa

Mtaalamu Maalumu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu, OHCHR Olivier De Schutter, ametuma amewataka Wakurugenzi Wakuu wa Amazon, DoorDash na Walmart kushughulikia madai kwamba mishahara katika mashirika haya yenye makao yake makuu nchini Marekani yanawaingiza wafanyakazi katika umaskini na kuwalazimisha kutegemea msaada wa serikali ya Marekani kuendesha maisha. 

Akina mama waleta watoto wao kwa uchunguzi wa lishe katika kliniki tembezi ya afya katika jimbo la Kassala, Sudan.
© UNICEF/Osman

Mamilioni hatarini kutokana na milipuko ya magonjwa Sudan: WHO

Sudan, nchi iliyoghubikwa na vita, hivi sasa inakabiliwa na janga lingine la afya ambapo magonjwa ya kipindupindu, surua, homa ya kidingapopo na malaria vinazunguka katika majimbo kadhaa na mchanganyiko wa magonjwa haya yote na utapiamlo vinaweza kuwa na athari mbaya sana kwa mamilioni ya watu limeonya leo shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO.