Nahisi nawajibika na kifo cha kila mlinda amani- Guterres
Umoja wa Mataifa na nchi zinazochangia kwenye operesheni za ulinzi wa amani wa chombo hicho leo wamekuwa na kikao cha ngazi ya juu kuangazia jinsi ya kuimarisha operesheni hizo.
Umoja wa Mataifa na nchi zinazochangia kwenye operesheni za ulinzi wa amani wa chombo hicho leo wamekuwa na kikao cha ngazi ya juu kuangazia jinsi ya kuimarisha operesheni hizo.
Mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ukianza leo, wakuu wa nchi na viongozi wa serikali wa nchi zinazochangia kwenye operesheni za ulinzi wa amani wanakutana kujadili jinsi ya kukabiliana na changamoto za ulinzi wa amani.
Kufuatia kutiwa saini kwa mkataba wa amani ulioboreshwa huko Sudan Kusini kati ya mahasimu wawili Rais Salva Kiir na makamu wake wa zamani Riek Machar, jopo la wataalamu limekutana huko Chuo Kikuu cha Juba kujadili kile kinachopaswa kufanyika ili kutekeleza mkakati huo huku wanachuo nao wakiwa na mtazamo wao.
Umoja wa Mataifa umezitaka pande kinzani nchini Sudan Kusini ziheshimu makubaliano mapya ya kusitisha mapigano ambayo pande hizo zilitia saini hivi karibuni ili kumaliza mapigano yaliyogubika nchi hiyo tangu mwezi disemba mwaka 2013. Assumpta Massoi na ripoti kamili.
Mlinda amani wa umoja wa mataifa anayehudumu kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini, UNMISS amejeruhiwa hii leo baada ya kupigwa risasi na askari wa jeshi la serikali nchini humo, SPLA.
Pengo kubwa la usawa kati ya ustawi wa binadamu unarudisha nyuma maendeleo ya ustawi wa binadamu, imesema ripoti mpya kuhusu kipimo cha maendeleo ya binadamu, HDI, iliyotolewa hii leo mjini New York, Marekani na shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP.
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa António Guterres amesema kusainiwa kwa mkataba ulioboreshwa ili kutatua migogoro nchini Sudan Kusini (RARCSS) tarehe 12 mwezi huu wa Septemba 2018 ni maendeleo mazuri na muhimu.
Ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu dhidi ya watoto nchini Sudan Kusini umesalia kuwa katika kiwango cha juu kisichokubalika huku takriban watoto 1,400 wakithibitishwa kuwa wahanga wa moja kwa moja wa ukiukwaji huo kwa mwaka 2017 na maelfu wengine wakiendelea kuteseka.
Uchunguzi wa mahakama ya kijeshi dhidi ya waliotekeleza uhalifu baada ya kushambulia Hotel ya Terrain mjini Juba nchini Sudan Kusini , umekamilika na hukumu kutolewa hii leo.
Wawakilishi wa wakimbizi nchini Sudan Kusini wamekutana ana kwa ana na pande kinzani katika mzozo wa Sudan Kusnini ambazo kwa sasa zinakutana mjini Khartoum Sudan kusaka suluhu ya mzozo huo.