Bonga bongo Sudan Kusini kuhusu mustakhbali wa mkataba wa amani

Mtu mwenye silaha katika mji wa Pibor, jimbo la Jonglei Sudan Kusini. Pibor umeshudia makabiliano yaliyosababisha watu kuhama na makazi yao kuharibiwa.
(Picha maktaba) OCHA/Cecilia Attefors
Mtu mwenye silaha katika mji wa Pibor, jimbo la Jonglei Sudan Kusini. Pibor umeshudia makabiliano yaliyosababisha watu kuhama na makazi yao kuharibiwa.

Bonga bongo Sudan Kusini kuhusu mustakhbali wa mkataba wa amani

Amani na Usalama

Kufuatia kutiwa saini kwa mkataba wa amani ulioboreshwa huko Sudan Kusini kati ya mahasimu wawili Rais Salva Kiir na makamu wake wa zamani Riek Machar, jopo la wataalamu limekutana huko Chuo Kikuu cha Juba kujadili kile kinachopaswa kufanyika ili kutekeleza mkakati huo huku wanachuo nao wakiwa na mtazamo wao.

Kwa  idadi kubwa ya vijana waliokuwa kwenye hadhira ya mjadala huo, ujumbe huu wa makubaliano ya amani ulikuwa ni hakikisho lakini fursa ya kufikia matarajio na ndoto zao vimesalia mikononi kwa wengine kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe, kuaminiana na kutekeleza mkataba huo.

Miongoni mwa vijana  hao ni Francis John mwanafunzi wa masuala ya fecha uhasibu katika Chuo hicho kikuu cha Juba ambaye amesema mkataba huo haumsumbui kwa kuwa si mara ya kwanza kufanyika..

 “Sudan Kusini imekuwa katika mizozo kwa kipindi cha miaka 21. Hawakufurahia amani hii. Ni vipi watafurahia amani hii? Ikiwa wanaweza kukaa pamoja, wale wa upinzani, na wa serikali pamoja na wananchi wote acha wakae pamoja  na wapiganie maendeleo ya taifa hili. Lakini bila watu hao kuwa pamoja na kuachana na maslahi yao tunaweza kupata amani, lakini bila hiyo itakuwa ngumu.”

Kwa upande wake Nyuol Justic Yaac, mwenyekiti wa tume ya haki za binamu nchini Sudan Kusini anasema…

  “Nadhani ni chaguo la watu wa Sudan Kusini kuukubali mkataba huo, hata ukiwa mbaya vipi,Ebu na tutafute njia ambazo zinaweza kutumiwa kuweza kuunyoosha . Naamini kuwa tuna uwezo wa kufanya hivyo. Kilichobaki ni vipi tutakuwa pamoja na tena lini na kuweza kuwa na jambo moja la pamoja la kupeleka mbele.”