Wakimbizi wa Sudan Kusini kushirikishwa katika mazungumzo ya amani.UNHCR

5 Septemba 2018

Wawakilishi wa wakimbizi nchini Sudan Kusini wamekutana ana kwa ana na  pande kinzani katika mzozo wa Sudan Kusnini ambazo kwa sasa zinakutana mjini Khartoum Sudan kusaka suluhu ya mzozo huo.

Katika taarifa iliyotolewa leo  na  shirika la Umoja wa Mataifa la UNHCR, mazungumzo ya Khartoum yatasaidia kuhakikisha kwamba sauti za wakimbizi zinaendelea kutoa mchango mkubwa katika juhudi za kuleta amani katika taifa ambalo limeghubikwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe.

UNHCR inasema kufuatia kurejelewa  kwa mazungumzo ya mkataba wa amani tangu Agosti 30,  wakimbizi 16 wa  Sudan Kusini kutoka mataifa sita wameketi pamoja na  makundi yanayohusika na mazungumzo mjini Khartoum. Wakimbizi hao wamewasili Kharthoum wakitekea Jamhuri ya Afrika ya Kati  CAR, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Ethiopia , Kenya , Uganda na Sudan ili kuelkezea mtazamo wao , matarajio na matumaini yao na pia kuwataka washiriki kusaka Amani kwa ajili ya mamilioni ya raia wa sudan kusini ,kama waoambao maisha yao yamesambaratishwa na vita.

Mazungumzo hayo ni hatua muhimu katika kusaka amani ya kudumu kwa watu wa Sudan kusini amesema Arnauld Akodjenou, mshauri maalumu wa Kamishina Mkuu wa wakimbizi kuhusu hali ya Sudan Kusini akisisitiza kuwa  “Ni muhimu sauti za wakimbizi zikasikika, kwani juhudi za ujenzi wa amani hazitomudu kuwapuuza wakimbizi.”

Tangu mugogoro huo   uanze mwaka 2013 takriban watu milioni 2.4 wamekimbia  Sudan Kusini, na sasa wanaishi kama wakimbizi huku wengine milioni 1.8 ni wakimbizi wa ndani nchini mwao.

Raia wengi wamekimbia ghasia , ukiukwaji wa haki za binadamu na mateso makali. Serikali ya Sudan pamoja na shirika la IGAD kwa ushirikiano na UNHCR na washirika wengine  ndio wanawasaidia na kufanikisha wajumbe hao wa wakimbizi kushiriki mazungumzo mjini Kharthoum Sudan.

Tags: UNHCR, IGAD, Sudan, Sudan Kusini, wakimbizi, mkutano wa amani.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter