TANZBATT-7 yatumia sanaa kuimarisha amani DRC
Sanaa katika operesheni za ulinzi wa amani zinazofanywa na Umoja wa Mataifa kwenye mataifa mbalimbali ikiwemo Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC imedhihirika kuwa mbinu muhimu ya kuleta utangamano miongoni mwa wanajamii wa taifa hilo hususan jimboni Kivu Kaskazini kwa kuwa na ujumbe maridhawa wa amani kwa rai na kusahau magumu wanayopitia kufuatia machafuko yaliyodumu kwa miongo kadhaa.