Vikundi vilivyojihami vyatesa jamii DRC, watu wauawa kwa kukatwa mapanga
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, limetoa wito kwa mamlaka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, ziimarishe uwepo wa jeshi na polisi kwenye maeneo ya mashariki mwa nchi hiyo ili kunusuru maisha ya raia wanaoendelea kuteseka na kuuawa na vikundi vilivyojihami.