Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

11 Machi 2022

11 Machi 2022

Pakua

Hii leo jaridani Flora Nducha anakuletea mada kwa kina inayomulika harakati za Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la chakula na kilimo FAO nchini Tanzania za kuwezesha wanawake kushiriki katika sekta ya uvuvi huko mkoani Kigoma kupitia mradi wa FISH4ACP ambako wanawake wamepaza sauti jinsi  ushiriki wao umesaidia kuinua kipato cha familia.
Pamoja na mada kwa kina kuna Habari kwa Ufupi zikimulika miaka 11 ya vita nchini Syria, huko Ukraine, UNHCR inaimarisha msaada wake nchini humo na nchi jirani kwa kuwa wakimbizi wanaendelea kusaka maeneo salama, na hatimaye ni Sudan Kusini ambako WFP inasema hali ya kibinadamu inazidi kuwa na changamoto kutokana na vita na mabadiliko ya tabianchi.
Kwenye kujifunza Kiswahili leo kutoka BAKIZA tunapata ufafanuzi wa methali, Undugu wa nazi hukutana chunguni. Karibu!
 

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
11'14"