Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

15 Machi 2022

15 Machi 2022

Pakua

Hii leo jaridani Leah Mushi anamulika: Hofu na shaka inayotawala kwa familia zilizoko ukimbizini ndani ya Ukraine huku waume au baba zao wakisalia kwenye mapigano; Wito wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kwa serikali Myanmar izuie vikosi vyake vya usalama kushambulia raia; Walinda amani wanawake wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania wakihudumu Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR wapaza sauti wanavyojisikia kuhudumu chini  ya bendera ya UN na mchango wao kwenye amani; Makala anabisha hodi kwenye kongamano la kimataifa la lugha ya kiswahili linaloendelea jijini Arusha nchini Tanzania na leo Mkurugenzi wa Radio Sauti ya Injili kutoka Goma, DRC anazungumza. Na kisha mashinani anabisha hodi Moldova kumulika harakati za Umoja wa Mataifa kufikisha misaada ya kiutu kwa wanawake na wasichana, karibu!

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
12'53"