Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

18 MACHI 2022

18 MACHI 2022

Pakua

Katika Jarida la mada kwa kina hii leo Ijumaa Lea Mushi na akuletea pamoja na mambo mengine

-Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani, WFP limesema wakati bei za vyakula duniani zimefikia kiwango cha juu kabisa, WFP ina wasiwasi  juu ya athari za vita nchini Ukraine katika uhakika wa upatikanaji chakula duniani.

-Mtaalamu Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya binadamu ya kupata maji safi na salama ya kunywa pamoja na huduma za kujisafi Pedro Arrojo Agudo ametaka kukomeshwa kwa tabia ya kujimilikisha, kuchafua na matumizi ya kupitiliza ya rasilimali ya maji ardhini ili kulinda haki ya binadamu ya kupata maji na kupunguza hatari zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi.

-Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na harakati za kutokomeza UKimwi, UNAIDS limepongeza bunge la Zimbabwe kwa hatua ya kufutilia mbali kifungu cha 79 cha sheria za uhalifu ambacho kinaharamisha maambukizi ya virusi vinavyosababisha UKimwi, VVU

-Katika  mada kwa kina leo tunaelekea nchini Tanzania, huko wadau wa idhaa za Kiswahili duniani wamekutana kuzungumza namna ya kuzidi kuitangaza lugha hiyo duniani

-Na kama ada ya kila Ijumaa tunajifunza Kiswahili leo mtaalam wetu Josephat Gitonga kutoka Kenya anafafanua maana ya methali "Mzoea kutwaa , kutoa ni vita"

 

 

 

Audio Credit
UN News/Leah Mushi
Audio Duration
16'52"