Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

LUGHA YA KISWAHILI KIMATAIFA

LUGHA YA KISWAHILI KIMATAIFA
Lugha ya kiswahili kuadhimishwa kimataifa kila tarehe 7 Julai - UNESCO

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO tarehe 23 mwezi Novemba mwaka 2021 lilitangaza rasmi tarehe 7 Julai ya kila mwaka kuwa siku ya Kiswahili duniani.

Maudhui ya maadhimisho ya mwaka huu ni Kiswahili kwa amani na ustawi. Lengo hasa la maadhimisho haya ya mwaka ni kusongesha matumizi ya lugha ya kiswahili kama nguzo ya amani, na ustawi na wakati huo kuimarisha tamaduni mbalimbali.

UNESCO ilipitisha uamuzi huo huko makao makuu yake mjini Paris Ufaransa wakati wa mkutano wa nchi wanachama wa shirika hilo.
Azimio lilipitishwa bila kupingwa na utekelezaji wake unaanza mwaka huu wa 2022.

Kupitia ukurasa huu mahsusi, utapataa taarifa zote kuanzia kupitishwa kwa azimio hilo, mapokeo yake na harakati za kukuza lugha ya Kiswahili ili iweze kujenga amani, uchumi, maendeleo na utangamano katika kona mbali mbali za dunia.

Utapata taarifa zilizochapishwa, video kutoka watu mbalimbali iwe maafisa wa serikali wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, maafisa wa UN wenyewe, wanazuoni, wanafunzi na wananchi wa kawaida.


 

22 Januari 2021

Leo Ijumaa ni mada kwa kina ikijikita katika harakati za  ukuzaji wa lugha ya kiswahili nchini Tanzania na nje ya mipaka hiyo kupitia kufundisha lugha hiyo adhimu wageni bila kusahau umuhimu wa kujumuisha watu wenye ulemavu katika harakati hizo. Hata hivyo tuna Habari kwa Ufupi ikimulika ukanda wa Sahel, Sudan na Syria na mwishoni ni maana ya sentensi na mchambuzi ni Aida Mutenyo kutoka Uganda. Mwenyeji wako leo ni Grace Kaneiya.

Sauti
9'56"
UN /Loey Felipe

Tunajitahidi kusongesha Kiswahili kwenye Umoja wa Mataifa

Lugha ya Kiswahili ambayo ni lugha ya kwanza ya kiafrika inayozungumzwa na watu wengi zaidi barani Afrika, ikiendelea kupokelewa na kutumiwa katika vyombo mbalimbali vya maamuzi kama vile kufanywa miongoni mwa lugha rasmi za SADC.

Assumpta Massoi amemhoji Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa, Balozi Profesa Kennedy Gastorn kuhusu juhudi za kuweza kukipa nafasi zaidi Kiswahili katika Umoja wa Mataifa. 

Sauti
1'49"
UNIC/Ahimidiwe Olotu

Tuzo za kimataifa za  lugha ya Kiswahili za Shaaban Robert kutolewa kesho Tanzania

Nchini Tanzania kesho Jumatano kunatolewa tuzo na nishani za kimataifa za lugha ya Kiswahili za Shaaban Robert. Tukio hilo litafanyika kwenye mji mkuu wa taifa hilo la Afrika Mashariki, Dodoma, ambapo tukio linaleta pamoja washiriki na manguli na wabobezi wa lugha ya Kiswahili kutoka maeneo mbalimbali duniani, na litahusisha pia viongozi waandamizi wa serikali na mashirika ya kitaifa na kimataifa. Lakini tuzo hizo zilianzia wapi? Na ni nini mantiki yake?

Sauti
6'

19 Januari 2021

Leo Jumanne tunamulika utoaji wa chanjo ya COVID-19 kwa wakimbizi huko Jordan, kisha tunakwenda Cameroon kumulika wakimbizi waliofurushwa kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR kutokana na machafuko nchini mwao. Huko Brazil tunamulika jinsi miti inatumika kufuta machozi ya familia zilizopoteza jamaa zao kutokana na COVID-19.

Sauti
12'29"
UN

Neno la Wiki: Maana ya Sentensi na aina zake

Leo Ijumaa ni wasaa wa kujifunza lugha ya Kiswahili. Na leo hii Mwenyekiti wa idara za Kiswahili katika Vyuo Vikuu Afrika Mashariki Aida Mutenyo akiwa Uganda anatufafanulia maana ya "Sentensi" Anataja aina sentensi kama vile za ombi au rai, sentensi sahili, ambatano na changamano.  Fuatana naye kwa kina katika uchambuzi huu ambao pia utaendelea Ijumaa ijayo.

Sauti
3'16"
UN

Neno la wiki-UZINZAJI

Katika kujifunza Kiswahili , leo tunapata ufafanuzi wa neno"UZINZAJI" na mchambuzi wetu ni   Onni Sigalla Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa  nchini Tanzania , BAKITA. 

Sauti
49"
UN

Neno la wiki-CHAZA

Katika kujifunza Kiswahili kupitia neno la wiki, leo tunapata ufafanuzi wa neno "CHAZA" na mchambuzi wetu ni   Onni Sigalla Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa  nchini Tanzania , BAKITA 

Sauti
40"