Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

19 Januari 2021

19 Januari 2021

Pakua

Leo Jumanne tunamulika utoaji wa chanjo ya COVID-19 kwa wakimbizi huko Jordan, kisha tunakwenda Cameroon kumulika wakimbizi waliofurushwa kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR kutokana na machafuko nchini mwao. Huko Brazil tunamulika jinsi miti inatumika kufuta machozi ya familia zilizopoteza jamaa zao kutokana na COVID-19. Katika makala Ahimidiwe Olotu anazungumza na Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi kutoka BAKITA kuhusu tuzo za kimataifa za kiswahili zitakazotolewa kesho jijini Dodoma nchini Tanzania na mashinani tunakwenda Jamhuri ya Afrika ya Kati, wachuuzi walalama kuwa machafuko nchini mwao yanakwamisha harakazi zao za kulisha familia. Karibu basi na mwenyeji wako ni Flora Nducha.

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
12'29"