Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

LUGHA YA KISWAHILI KIMATAIFA

LUGHA YA KISWAHILI KIMATAIFA
Lugha ya kiswahili kuadhimishwa kimataifa kila tarehe 7 Julai - UNESCO

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO tarehe 23 mwezi Novemba mwaka 2021 lilitangaza rasmi tarehe 7 Julai ya kila mwaka kuwa siku ya Kiswahili duniani.

Maudhui ya maadhimisho ya mwaka huu ni Kiswahili kwa amani na ustawi. Lengo hasa la maadhimisho haya ya mwaka ni kusongesha matumizi ya lugha ya kiswahili kama nguzo ya amani, na ustawi na wakati huo kuimarisha tamaduni mbalimbali.

UNESCO ilipitisha uamuzi huo huko makao makuu yake mjini Paris Ufaransa wakati wa mkutano wa nchi wanachama wa shirika hilo.
Azimio lilipitishwa bila kupingwa na utekelezaji wake unaanza mwaka huu wa 2022.

Kupitia ukurasa huu mahsusi, utapataa taarifa zote kuanzia kupitishwa kwa azimio hilo, mapokeo yake na harakati za kukuza lugha ya Kiswahili ili iweze kujenga amani, uchumi, maendeleo na utangamano katika kona mbali mbali za dunia.

Utapata taarifa zilizochapishwa, video kutoka watu mbalimbali iwe maafisa wa serikali wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, maafisa wa UN wenyewe, wanazuoni, wanafunzi na wananchi wa kawaida.


 

UN News Kiswahili

Neno la Wiki: Mchirizi na Mtaro

Katika neno la wiki hii leo tunabisha hodi, Baraza la Kiswahili Zanzibar, BAKIZA ambako mchambuzi wetu  Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo anafafanua maana ya maneno MTARO na MCHIRIZI.

 

Sauti
49"
UN News Kiswahili

Neno la Wiki-NASIHA

Na sasa ni muda wa kujifunza Kiswahili na leo mchambuzi wetu kutoka Baraza la Kiswahili Tanzania , BAKITA ni Onni Sigalla Mhariri mwandamizi anafafanua maana ya neno "NASIHA"

Sauti
41"
UN News Kiswahili

Kiswahili chazidi kupasua mawimbi ya bahari na mawingu hata ughaibuni

Kiswahili! Kiswahili! Kiswahili! Kinazidi kupasua mawimbi ya bahari na mawingu na kuwa kivutio siyo tu kwa watu wazima bali pia watoto wadogo tena ughaibuni.

Huyu ni Braydon Bent, mchambuzi wa soka pengine mdogo zaidi barani Ulaya akijinasibu kwa lugha ya Kiswahili na kuleta msisimko mkubwa kwa mashabiki wake. Mwenzangu Arnold Kayanda amezungumza na mwalimu wa Kiswahil wa Braydon aitwae John Jackson hivi sasa mkazi wa Ujerumani akianza kwanza kwa kuelezea kilichomvutia na Kiswahili.

Sauti
5'43"
UNHCR/Catherine Wachiaya

Walimu wa Kiswahili wamekiri kitabu changu kiliwashawishi kuthamini lugha hiyo adhimu- Walibora

Shirika la elimu sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa, UNESCO limekuwa katika mstari wa mbele katika kuchagiza kuwepo kwa dunia yenye watu wanaojua kusoma na kuandika. UNESCO kwa mtazamo wake unachukulia kupata stadi na kuimarisha stadi hizo za kusoma na kuandika katika maisha kama sehemu muhimu ya haki ya elimu. Matokeo yake yakiwa ni kuwawezesha watu kushiriki kikamilifu katika jamii na kuchangia katika kumarisha maisha yao.

Sauti
4'6"
UN News Kiswahili

Neno la Wiki- Methali Kandamizi kwa wanawake

Hii leo katika NENO LA WIKI, Mwenyekiti wa idara za Kiswahili katika vyuo vikuu Afrika Mashariki Aida Mutenyo  anatufafanulia methali za Kiswahili ambazo kwa mtazamo wake zinamkandamiza mwanamke katika jamii. 

  1. Mwanamke ni kama ardhi, yeyote anaweza kukaa.

  2. Mwanamke ni bustani na mwanaume ni uzio

  3. Mwanamke mpumbavu huvunja nyumba yake kwa mikono yake!

  4. Mke hafikirii zaidi ya kitanda anacholala!

  5. Maneno kwa mwanamke matendo kwa mwanaume!

Sauti
6'25"
UN News

Ufahamu wa Kiswahili wamwinua mwananchi wa Uganda miongoni mwa wakimbizi

Lugha ya Kiswahili imeendelea kusambaa na kukita mizizi hata katika maeneo ambayo hapo awali haikuwa na nguvu. Na kuenea kwa lugha hiyo adhimu kunachagizwa na matukio tofauti tofauti iwe amani na hata wakati mwingine mizozo. Ni katika mazingira kama hayo ambapo mwananchi wa Uganda Nsungwa Anette Khadja ameitumia fursa ya uhitaji wa lugha ya Kiswahili katika kambi ya wakimbizi ya Kyangwali wilayani Hoima nchini humo kwa kujifunza Kiswahili na sasa anafundisha lugha hiyo kwa wanafunzi wakimbizi na wenyeji.

Sauti
3'44"
UN News Kiswahili

Neno la Wiki: Aghalabu

Katika kujifunza Kiswahili, Mchambuzi Onni Sigalla wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania “BAKITA” anachambua maana na matumizi ya neno “AGHALABU” ambapo anaeleza maana mbili za neno hilo. Tofauti na ile iliyozoeleka kwa matumizi ambapo neno aghalabu hutumiwa kueleza utokeaji wa mara kwa mara wa jambo, mtaalam huyo ameongeza maana nyingine isiyofahamika sana inayohusishwa na kundi la watu katika jamii au jumuiya.

Sauti
1'1"