Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

LUGHA YA KISWAHILI KIMATAIFA

LUGHA YA KISWAHILI KIMATAIFA
Lugha ya kiswahili kuadhimishwa kimataifa kila tarehe 7 Julai - UNESCO

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO tarehe 23 mwezi Novemba mwaka 2021 lilitangaza rasmi tarehe 7 Julai ya kila mwaka kuwa siku ya Kiswahili duniani.

Maudhui ya maadhimisho ya mwaka huu ni Kiswahili kwa amani na ustawi. Lengo hasa la maadhimisho haya ya mwaka ni kusongesha matumizi ya lugha ya kiswahili kama nguzo ya amani, na ustawi na wakati huo kuimarisha tamaduni mbalimbali.

UNESCO ilipitisha uamuzi huo huko makao makuu yake mjini Paris Ufaransa wakati wa mkutano wa nchi wanachama wa shirika hilo.
Azimio lilipitishwa bila kupingwa na utekelezaji wake unaanza mwaka huu wa 2022.

Kupitia ukurasa huu mahsusi, utapataa taarifa zote kuanzia kupitishwa kwa azimio hilo, mapokeo yake na harakati za kukuza lugha ya Kiswahili ili iweze kujenga amani, uchumi, maendeleo na utangamano katika kona mbali mbali za dunia.

Utapata taarifa zilizochapishwa, video kutoka watu mbalimbali iwe maafisa wa serikali wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, maafisa wa UN wenyewe, wanazuoni, wanafunzi na wananchi wa kawaida.


 

03 JULAI 2020

Mada kwa kina inamulika lugha ya Kiswahili na ulinzi wa amani huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Mjini Beni, jimboni Kivu Kaskazini ambako walinda amani kutoka Tanzania wanahudumu chini ya bendera ya Umoja wa Mataifa. Wanafanya kazi kwenye kikosi maalum cha kujibu mashambulizi kilichoanzishwa na azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa namba 2098  tarehe 28 mwezi Machi mwaka 2013. Mwenyeji wetu wa kutufafanulia uhusiano wa amani na lugha ya Kiswahili ni Luteni Issa Mwakalambo, Afisa habari wa kikosi cha Tanzania, TANZBATT 7. 

Sauti
9'58"

23 JUNI 2020

Ikiwa leo ni siku ya wajane duniani Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametaka kuangaziwa zaidi kwa kundi linalosahaulika mara kwa mara, wajane, hususan wakati huu wa janga la ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19. Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na mkuu wa mpango wa Umoja huo nchini Somalia UNSOM, James Swan amesema ms

Sauti
14'9"
UN News Kiswahili

Neno la Wiki-Ujana ni moshi

Sasa  ni Neno la wiki ambapo leo tutajifunza maana ya methali "Ujana ni Moshi" na mchambuzi wetu Josephat Gitonga, mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi katika kituo cha tafsiri na ukalimani 

Sauti
57"

24 APRILI 2020

Katika Jarida la Habari hii leo Flora Nducha anakuletea

-Mwezi mtukufu wa Ramadhani unaanza leo kote duniani Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa awatakia kila la heri Waislam wote na kusema kwamba COVID-19 itaifanya Ramadhan ya mwaka huu kuwa tofauti kabisa

-Kamishina Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet amesema anatiwa hofu na kamatakamata na kubanwa kwa vyombo vya habari wakati huu wa janga la COVID-19 ambapo taarifa sahihi ni muhimu sana

Sauti
10'46"