Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanaoishi katika makazi duni wanahitaji mnepo dhidi ya mabadiliko ya tabianchi:UN-HABITAT

Wanaoishi katika makazi duni wanahitaji mnepo dhidi ya mabadiliko ya tabianchi:UN-HABITAT

Pakua

Mamilioni ya watu wanaoishi katika mitaa ya mabanda au makazi dunia kote duniani wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo miundombinu mibovu, ukosefu wa maji safi na salama n ahata hali mbaya ya Maisha lakini kubwa zaidi kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la makazi duniani UN-HABITAT ni kutokuwa na mnepo wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi. Shirika hilo linasema vimbunga au mafuriko yanapozuka wao huwa wa kwanza kuathirika na hasara yake ni kubwa Zaidi kuliko wengine. Kwa kutambua hilo sasa UN-HABITAT kwa kushirikiana na serikali mbalimbali duniani, wataalam wa miundombinu na wasanifu majengo wa kupitia ufadhili wa Benki ya Dunia wameanzisha program maalum ya kuwajengea mnepo watu hao ambao asilimia kubwa ni masikini. Kupata undani zaidi ungana na Grace Kaneiya katika Makala hii ya mabadiliko ya tabianchi.

Audio Credit
Loise Wairimu/Grace Kaneiya
Audio Duration
4'8"
Photo Credit
UN-Habitat/Nathan Kihara