Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakunga wapaza sauti kuhusu changamoto kazini

Wakunga wapaza sauti kuhusu changamoto kazini

Pakua

Wakunga na wauguzi huwa msitari wa mbele kwenye shughuli nyingi za kitabibu na hivyo huchangia sehemu muhimu ya huduma za afya.

Lakini licha ya hayo mara nyingi hulaumiwa na umma wakidai wanazembea kuwahudumia sanjari na matarajio.

Kazi zote kawaida huwa na mapungufu ambayo ni vyema yashughulikiwe kwa njia za amani kwa kujadiliana badala ya kulaumiana, ndivyo wanavyosema wakunga nchini Uganda kwenye mkutano wa wadau uliokuwa motomoto ukisaka njia za kuboresha huduma za afya.

Je, wakunga wanasema nini? na  wanataka nini? Basi ungana na John Kibego kukujuza zaidi katika makala ifuatayo.

Audio Credit
Loise Wairimu/ John Kibego
Audio Duration
3'42"
Photo Credit
UNFPA