Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabaya mengi yanayosemwa kuhusu wakunga/wauguzi sio- Bi. Mafuru

Mabaya mengi yanayosemwa kuhusu wakunga/wauguzi sio- Bi. Mafuru

Pakua

Wakati dunia ikiwa katika muongo wa mwisho kuelekea kutimiza malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa yenye ukomo wake mwaka 2030, kuna mwamko mpya kwa nchi wanachama kutimiza malengo hayo ikiwemo lengo namba Tatu la afya kwa wote. 

Katika kufanikisha lengo hilo, wakunga na wauguzi wana mchango mkubwa kwani afya ya uzazi ni moja ya sekta ambazo bado inakabiliwa na changamoto ikiwemo nguvu kazi.  

Katika makala hii Stella Vuzo wa Kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa, Dar es Salaam nchini Tanzania ambaye amezungumza na Furaha Mafuru kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu duniani, UNFPA nchini humo kitengo cha mama na mtoto ambaye anaanza kwa kueleza kuhusu takwimu za idadi wanaosaka huduma ya hospital wakati wa kujifungua

Audio Credit
Anold Kayanda/Stella Vuzo
Audio Duration
3'56"
Photo Credit
© UNICEF/Karel Prinsloo