Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nilivutiwa kuwa muuguzi kwa sababu mama yangu alikuwa muuguzi-Jackline Ayuma

Nilivutiwa kuwa muuguzi kwa sababu mama yangu alikuwa muuguzi-Jackline Ayuma

Pakua

Wakati dunia ikiadhimisha mwaka wa wakunga na wauguzi, shirika la afya ulimwenguni limesema nguvu kazi thabiti ya kundi hilo ni muhimu katika kufikia afya kwa wote.

Hatahivyo, WHO imesema mara nyingi wauguzi na wakunga hawathaminiwi na hushindwa kufikia uwezo wao kamili. Mwaka 2020 tunalenga kuhakikisha kwamba wauguzi na wakunga wanafanya kazi katika mazingira ambayo ni salama, wanakoheshimiwa na wafanyakazi wenzao na wanajamii na kwmaba wanafikia huduma ya afya na wanakofanyia kazi wanajumuishwa na wataalam tofauti wa kiafya.

Katika Makala hii Saa Zumo wa radio washirika Pangani FM ya Tanga Tanzania, amezungumza na muuguzi/ mkunga akiwa hospitali ya Pangani, kwanza anaanza kwa kujitolea.

Audio Credit
UN News/Saa Zumo
Audio Duration
2'41"
Photo Credit
UNFPA Mozambique