Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Fahamu jinsi Nukta Fakti ilivyosaidia lishe bora kwa watoto kupitia mtandao

Fahamu jinsi Nukta Fakti ilivyosaidia lishe bora kwa watoto kupitia mtandao

Pakua

Leo katika makala tunakwenda Tanzania kuzungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya habari na teknolojia ya Nukta Afrika Nuzulack Dausen  ambaye pia mwanzilishi wa Jiko point inayojihusisha zaidi na utoaji habari sahihi kuhusu uhakika wa chakula na lishe, jambo ambalo linapigiwa upatu kila uchao na Umoja wa Mataifa. Amezungumza hivi karibuni jijini Dar es Salaam na Stella Vuzo afisa habari wa Umoja wa Mataifa kufahamu kwa undani wanachokifanya katika kutimiza azma hiyo na anaanza kwa kueleza Jiko point ni nini hasa?

Audio Credit
Assumpta Massoi/Flora Nducha
Audio Duration
3'22"
Photo Credit
FAO Tanzania