Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

UN News/Ziad Taleb

Huku wanakimbia vita wanawake wa Gaza inakuwaje wakiwa katika hedhi?

Kunapozuka mizozo na machafuko wananchi wote wanaathirika kwasababu maisha yao yanaparanganyika kabisa tofauti na walivyokuwa wamezoea. Watoto waliokuwa wakienda shule sasa hawaendi, si wafanyabiashara, wakulima wala viongozi wa dini wanaotekeleza majukumu yao ya kila siku na suala moja lililo kweli kwa kila mtu ni kuwa wanatafuta kila namna ya kuokoa maisha yao na wengi njia hiyo huwa ni kukusanya virango vyao kidogo wanavyoweza kubeba na kukimbia kuokoa nafsi zao. 

Sauti
4'35"
Redio Domus/Kevin Keitany

Redio ni chombo cha mawasiliano kilicho rafiki

Licha ya redio ambacho ni chombo cha kuaminiwa kwa miaka mingi katika usambazaji wa taarifa, kukabiliwa na changamoto nyingi katika nyakati hizi ambazo kuna utitiri wa teknolojia za usambazaji wa habari, bado inaonekana watu wana imani kubwa na chombo hiki kwa sababu mbalimbali. Wachache kati ya wengi, ni wadau hawa tuliozungumza kutoka Afrika Mashariki. Kwanza ni Rose Haji, mwanahabari mwandamizi wa siku nyingi nchini Tanzania akieleza kuhusu kazi kuu za redio.

Sauti
3'28"
© WFP/Eulalia Berlanga

Benki ya Maendeleo ya Afrika na UNHCR waungana kusaidia wakimbizi nchini Sudan Kusini

Vita vinapotokea wananchi wanalazimika kusaka kila namna ya kujilinda na kuokoa maisha yao. Mambo yanapokuwa mabaya watu hao hulazimika kuacha kila kitu nyuma na kukimbia kwenda kusaka hifadhi sehemu nyingine. Watu hao wanapoondoka wanaondoka na ujuzi wao mfano kama alikuwa muuguzi, mfanya biashara, fundi muashi au taaluma yoyote ile. 

Mara nyingi sehemu wanazofikia wakimbizi hao iwe ndani au nje ya nchi zao hujikuta wakipata mahitaji muhimu kwa ajili ya kuishi kama vile chakula cha msaada na matibabu, kiufupi watu hawa hugeuka kuwa tegemezi. 

Sauti
3'47"
11-12-2023_FAO_Lopit_South Sudan.jpg

FAO yawashika mkono wasichana Afrika kuingia katika sayansi ya kilimo

Katika kuelekea siku ya kimataifa ya wanawake na wasichana katika sayansi itakayoadhimishwa Jumapili Februari 11 shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO limesema katika Dunia ya sasa inayobadilika kwa kasi, sayansi na ubunifu vina jukumu muhimu katika kushughulikia changamoto zinazoiandama Dunia.

Sauti
4'15"
UNDP/Tanzania

Kampeni ya UNDP Tanzania ya kukabili misimamo mikali yainua vijana kiuchumi Kilwa Masoko mkoani Lindi

Nchini Tanzania, shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP linatekeleza mradi wa kukabili misimamo mikali kupitia kampeni ya amani kama njia mojawapo ya kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Tayari kuna wanaufaika na mmoja wao ni Nuru Mbaruku Ramadhani, mwenyekiti wa kikundi cha Masoko 2 Peace Club kilichoko Kilwa Masoko mkoa wa Lindi, kusini mashariki mwa Tanzania. Kikundi hiki kilichoanzishwa mwezi Juni mwaka 2023, kina mabalozi 9 wa amani wakiwemo wanawake 6 na wanaume 3.

Sauti
5'1"
UN Habitat Mozambique

Mwanafunzi Msumbiji: Iwe mvua iwe upepo mkali madarasa yetu ni salama

Kila mwaka, Msumbiji hukabiliwa na matukio ya hali mbaya za hewa kupindukia kama vile vimbunga na mafuriko, matukio ambayo husababisha uharibifu wa shule na hatimaye watoto kushindwa kujifunza. Hata hivyo, ujenzi wa madarasa yanayohimili matukio kama vile pepo kali na mafuriko umeleta nuru na matumiani kwa watoto, wazazi na walimu. Madarasa haya yanawezesha watoto kubakia salama hata wakati wa mvua na upepo mkali. Hali hii ni uwekezaji wa kudumu kwani ni  hakikisho kwa watoto kuendelea kupata elimu na mustakabali wao kuwa bora.

Sauti
4'11"
© FAO/IFAD/WFP/Eduardo Sotera

Angola: Mradi wa IFAD umeniheshimisha Kijiji kwetu- Albertina

Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo, IFAD ni taasisi ya fedha ya kimataifa na pia shirika la Umoja wa Maitafa lililojikita katika kutokomeza umaskini na njaa kwenye maeneo ya vijijini yaliyoko katika nchi zinazoendelea. Miongoni mwa maeneo ambako Mfuko huo unafanya kazi ni nchini Angola barani Afrika ambako huko takwimu zinaonesha ongezeko la vijana wanaohamia mijini kutoka vijijini kwa sababu ya umaskini wa vijijini.

Sauti
4'36"
World Bank

Nuzulack Dausen: Nishati safi inanusuru mazingira na kuinua kipato katika jamii

Leo ni siku ya kimataifa ya nishati safi ambayo lengo lake ni kuzihimiza jamii kote duniani kutekeleza lengo la 7 la maendeleo la Umoja wa Mataifa la kuhakikisha kila mtu anahamia kwenye matumizi ya nishati hiyo ifikapo mwaka 2030. Nchini Tanzania wako msitari wa mbele katika harakati za utekelezaji wa lengo hilo na miongoni mwao ni Nuzulack Dausen mwanzilishi wa Jukwaa la kidijitali la Jiko point linaloendesha kipindi cha mwanaume jikoni kupitia mtandao wa Youtube.

Sauti
5'1"