Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

Video ya UN

Tumeanza na gari la betri za kuchaji lakini tunaelekea kwenye nishati ya jua – Masoud Kipanya 

Katikati ya mwezi huu, Julai 17, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akihutubia kongamano kubwa la uchumi kuhusu nishati na tabianchi mjini Washington DC, nchini Marekani,  ameonya kwamba mwenendo wa sasa wa uchumi wa dunia ambao unajikita zaidi katika matumizi ya rasilimali kama mafuta kisukuku utaongeza zahma ya mfumuko wa bei, changamoto ya mabadiliko ya tabianchi na vita. 

Sauti
6'3"
TANZBATT9

Walinda amani wa UN kutoka Tanzania walenga kuhamasisha amani DRC kupitia Kiswahili 

Kikundi cha tisa cha walinda amani kutoka Tanzania, TANZBATT-9, kinachohudumu chini ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO kimeanza kusambaza daftari na vifaa vingine vya shule kwa watoto katika maeneo ya Mavivi huko BENI mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa lengo la kuwahimiza wanafunzi hao kuzungumza lugha ya Kiswahili ili wakimaliza shule waweze kuwasiliana na mataifa mengine.

Sauti
4'27"
TANZBATT 9

Lugha ya Kiswahili inatusaidia sana kwenye ulinzi wa amani DRC- Luteni Kanali Mley 

Lugha ya Kiswahili hivi sasa ni lugha ya kimataifa ikiwa imetengewa siku yake mahsusi ya kuadhimishwa ambayo ni tarehe 7 Julai kila mwaka. Wakati wa maadhimisho ya mwaka huu, Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO, Audrey Azoulay alisema uamuzi wa Baraza Kuu la UNESCO kutambua lugha ya kiswahili kimataifa ulizingatia mambo kadhaa ya msingi ikiwemo nafasi ya lugha hiyo katika kusongesha amani.

Sauti
3'49"
UN News

Stadi za maisha ni muhimu hususani kwa vijana ili kufikia malengo ya maendeleo endelevu

Nchini Tanzania Jumla ya Kaya 13,600 na vijana 2,700 wanatarajiwa kunufaika na tathmini ya upimaji stadi za maisha kwa kuangalia viwango vyao vya kujitambua, ushirikiano walionao kwao na kwa jamii, jinsi wanavyotatu matatizo pamoja na heshima binafsi jinsi wanavyojiheshimu wao, jamii na mali za wengine. Sifa zote hizo ni muhimu katika kusaidia wanajamii wa rika mbalimbali wanashiriki katika kufanikisha Malengo ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endelevu, SDGs. 

Sauti
4'8"
© UNFPA/Joseph Scott

Kampeni ya M’mera mpoyamba yasaidia SDG3 Malawi

Katika kusongesha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs likiweno lengo namba 3 linalolenga Afya bora na ustawi, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini Malawi linaendesha kampeni ya M’mera mpoyamba inayohamasisha wajawazito kufika katika vituo vya afya angalau mara nne kabla ya kujifunga na kuhakikisha wanapata saa moja ya ziada ya kulala ili kujihakikishia ujauzito salama na kujifungua mtoto mwenye afya bora.

Sauti
2'56"
FAO Tanzania

Mafunzo ya ujuzi yaliyofadhiliwa na ILO yamenikwamua kwenye biashara yangu ya chakula – Hamad Hamis

Mwaka 2014, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilitangaza tarehe 15 Julai kuwa Siku ya Stadi kwa Vijana Duniani, ili kusherehekea umuhimu wa kimkakati wa kuwapa vijana ujuzi wa kuajiriwa, kazi zenye staha na ujasiriamali. Tangu wakati huo, Siku ya Stadi kwa Vijana Duniani imetoa fursa ya kipekee ya mazungumzo kati ya vijana, taasisi za elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi (TVET), makampuni, waajiri na mashirika ya wafanyakazi, watunga sera na washirika wa maendeleo.  

Sauti
3'29"
UN/Assumpta Massoi

Lugha ya Kiswahili imenipa ajira Umoja wa Mataifa

Kutana na Priscilla Lecomte, mtaalamu wa mawasiliano wa UN-CBi, mpango unaoratibiwa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura, OCHA na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo duniani, UNDP kushirikisha sekta binafsi katika kujiandaa kukabliana na majanga na hata kurejea katika hali nzuri baada ya majanga. Bi.

Sauti
2'31"
UNFPA Video

Nafurahi sana ninapoona mjamzito kajifungua salama- Mkunga Erika

Umoja wa Mataifa hii leo umetoa ripoti yake kuhusu idadi ya watu ambapo idadi ya watu duniani inatarajiwa kuongezeka na kufikia bilioni 8 tarehe 15 mwezi Novemba mwaka huu wa 2022. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake wa siku hii anaweka bayana kuwa ongezeko hilo la idadi ya watu linatokana na sababu kadhaa ikiwemo maendeleo makubwa katika huduma za afya, maendeleo ambayo  yamechochea pia kupungua kwa vifo vya wajawazito na watoto wachanga.

Sauti
3'33"