Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania yazindua programu ya malezi, ustawi na makuzi ya watoto katika mikoa 10

Tanzania yazindua programu ya malezi, ustawi na makuzi ya watoto katika mikoa 10

Pakua

Lishe duni ni moja ya changamoto mtambuka hususani katika ustawi na makuzi ya watoto. Kwa kulizingatia hilo na kwa kutambua kuwa kila nchi inapaswa kushiriki katika kuyasongesha malengo ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endekevu, SDGs, Tanzania imezindua programu jumuishi ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto kwa lengo la kumaliza changamoto ya lishe duni na changamoto nyingine dhidi ya watoto hususani walio chini ya umri wa miaka nane. Pamoja na mambo mengine, lishe duni inachangia kwa kiasi kikubwa kukwamisha lengo namba 3 kwa kuwakosesha watoto afya bora, na lengo namba 4 kwa kuwa kikwazo katika ujifunzaji wao. Hamad Rashid mwandishi kutoka Redio washirika wetu Tanzania kidstime, amehudhuria uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Morogoro na kuandaa makala ifuatao.

Audio Credit
Anold Kayanda/Hamad Rashid
Audio Duration
3'37"
Photo Credit
UN Women/Ruth McDowall