Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sabrina Elba, Balozi mwema wa IFAD, aona jinsi miradi yanufaisha vijana kaunti ya Nyeri Kenya 

Sabrina Elba, Balozi mwema wa IFAD, aona jinsi miradi yanufaisha vijana kaunti ya Nyeri Kenya 

Pakua

Mabadiliko ya tabianchi yanayoendelea kukumba Dunia kila uchao hayajaacha wakulima salama. Nchini Kenya, wakulima vijana katika kaunti ya Nyeri, miaka miwili iliyopita walitegemea mto wa jirani na maji ya mvua kumwagilia mashamba yao ya mboga za majani. Hata hivyo ukame na mvua zisizotabirika vilivyosababishwa na mabadiliko ya tabianchi vilikatisha wakulima tamaa. Lakini Umoja wa Mataifa kupitia mfuko wake wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo, IFAD ulisikia kilio cha wakulima hao vijana na kupatia fedha mashirika mawili:  KCEP CRAL linalohusika na programu ya kuboresha nafaka na mnepo pamoja na UTanRMP la usimamizi wa bonde la mto Tana ambao waliwezesha wakulima kupatiwa vifaa ikiwemo vya umwagiliaji. Sasa hali ni shwari kwa vipi? Ungana na Assumpta Massoi katika makala hii. 

Audio Credit
Grace Kaneiya/Assumpta Massoi
Sauti
4'9"
Photo Credit
Video ya IFAD