Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

© Unsplash/Possessed Photograph

Mauritius waelekeza mbinu wanazotumia kutokomeza uvutaji wa tumbaku nchini mwao

Mwishoni mwa mwezi Julai mwaka huu shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya Afya WHO walitoa ripoti ya 9 kuhusu janga la uvutaji tumbaku na kueleza kuwa mafanikio yameanza kuonekana kwa nchi wanachama kutekeleza sera ya kulinda umma kutoathirika na uvutaji wa sigara unaofanywa na mtu mwingine ambapo zaidi ya watu bilioni 5.6 wamenufaika na sera hiyo ulimwenguni kote. Nchi ya Mauritius ilipongezwa kwa kuwa nchi pekee iliyotekeleza vyema sera zote sita za kupambana na athari za tumbaku. Je waliwezaje?

Sauti
3'54"
UN Brazil

Amina J. Mohammed ziarani Amazon: Nimesikia maombi yenu na tutapaza sauti

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed anaendele ana ziara yake ya siku tano nchini Brazil ambapo siku ya Alhamisi Agosti 3, 2023 alizuru jamii ya watu wa asili ya Mapuera kwenye ukanda wa Amazon jimboni Para ambako huko alipata fursa ya kuzungumza na wanajamii hao na kusikia maombi yao, ziara ambayo anafanya kufuatilia utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs kuelekea mkutano wa viongozi kuhusu SDGs mwezi Septemba mwaka huu. Thelma Mwadzaya anatusimulia kilichojiri. 

Sauti
3'46"
©FAO/IFAD/WFP/Eduardo Soteras.

Maji ya kisima hiki ni jawabu kwa afya na kipato – Mwananchi Sudan Kusini

Kwa siku tatu, viongozi wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa, lile la Mpango wa Chakula (WFP), Chakula na Kilimo (FAO) na Mfuko wa Maendeleo ya Kilimo duniani, IFAD walikuwemo nchini Sudan Kusini kuona ni kwa jinsi gani miradi wanayotekeleza kwa pamoja ya kujenga mnepo na kuhakikisha lishe ya uhakika na bora imeleta mabadiliko. Wakazi wa Apada Boma jimboni Bahr el Ghazal Kaskazini nchini humo walikuwa taswira ya manufaa ya miradi hiyo ambayo wakuu hao walikagua kama inavyofafanua Makala hii iliyoandaliwa na Assumpta Massoi. 

Sauti
4'18"
UNDP Zimbabwe

Je unafahamu kuwa kuna fursa ya ufadhili katika nishati safi na salama Tanzania?

Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la mfuko wa maendeleo ya mitaji UNCDF wakizingatia Utafiti wa Bajeti ya Kaya Tanzania Bara (2017/18), upatikanaji wa nishati safi na teknolojia ya kupikia ni asilimia 17.1 tu ya wakazi wa mijini na asilimia 2 ya wakazi wa vijijini. Kuongezeka kwa mahitaji ya nishati ya kuni kunatokana na ukuaji wa haraka wa miji, bei ya juu, na upatikanaji mdogo wa nishati mbadala.

Sauti
5'22"
Credit: UN/Assumpta Massoi

Kutoka Dodoma Tanzania Bara hadi Paje, Zanzibar kukabiliana na  umaskini

Moja ya malengo ya Umoja wa Mataifa kuhusu maendeleo endelevu, SDGs ni kutokomeza umaskini ifikapo mwaka 2030. Ikiwa imesalia miaka 7 kabla ya kufikia ukomo, nchi, jamii na kila mtu mmoja mmoja anachukua hatua kutokomeza umaskini hasa kuanzia ngazi ya familia. Umaskini unasababisha watu washindwe sio tu kupata mlo bali pia kupeleka watoto wao shuleni kupata elimu bora.

Sauti
3'36"
UNHCR Video

Kutana na Timu ya Taifa ya Kandanda ya Wanawake ya Afghanistan - Wakimbizi katika Michezo

“Tunajaribu kuleta michezo na nguvu zake katika mazingira magumu sana ya watu wasiojiweza. Mchezo ni mzuri kwa kuwapa watu matumaini ya siku zijazo.” Anasema Filippo Grandi, Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) akirejelea Timu ya mpira wa miguu ya wanawake wakimbizi wanaoishi nchini Australia baada ya kuokoa maisha yao yaliyokuwa hatarini nchini mwao Afghanistan. Anold Kayanda anasimulia zaidi. 

Sauti
4'17"
UN/Eugene Uwimana

WD2023 imeonesha kuwa wanawake tunachukua hatua mashinani - Martha Wanza

Mkutano wa kimataifa wa Women Deliver 2023 (WD2023) au wanawake wanatekeleza umekunja jamvi mwishoni mwa wiki mjini Kigali nchini Rwanda baada ya kuwaleta pamoja washiriki 6,000 ana kwa ana na wengine zaidi ya 200,000 mtandaoni. Lengo kuu la mkutano huo mkubwa kabisa uliozanza Julai 17 hadi 20 na kubeba kaulimbiu “Nafasi, mshikamano na suluhu” lilijikita katika ujumuishwaji ili kusongesha usawa endelevu wa kijinsia kwa kuhusisha sekta mbalimbali.

Sauti
4'8"
UN News/George Musubao

Asante UNMAS kwa kutegua bomu lililotishia uhai wetu- Wananchi Kididiwe, DRC

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo - DRC, Shirika la Umoja wa Mataifa la kutegua Mabomu ya ardhini (UNMAS) Jumanne Julai 18 mwaka huu wa 2023  lilitegua bomu lenye uzito wa kilo 250 lililogunduliwa wiki iliyopita na wakulima katika eneo la Kididiwe, wilayani Beni. Jimboni Kivu Kaskazini. Wakazi wanaonesha furaha yao kwa Umoja wa Mataifa kwa kutegua bomu hilo linalosababisha vifo.  Mwandishi wetu wa nchini DRC, George Musubao amefuatilia na kuandaa makala hii. 

Sauti
3'55"
Stella Vuzo/UNIC Dar es

Sauti za asasi za kiraia katika utekelezaji wa SDGs ni muhimu: UNA

Jukwaa la ngazi ya juu la kisiasa la Umoja wa Mataifa kuhusu malengo ya maendeleo endelevu HLPF, linaendelea hapa Makao Makuu jijini New York Marekani likitathimini utekelezaji wa malengo hayo yaliyosaliza chini ya miaka 7, kabla ya kufikia ukomo hapo mwaka 2030. Mbali ya tathimini ya utekelezaji wake jukwaa hilo limetoa fursa kwa nchi 39 zilizojitolea kuwasilisha ripoti za kitaifa za utekelezaji wa malengo hayo. Tanzania ni miongoni mwa nchi hizo na iliwasilisha ripoti yake jana Jumanne.

Sauti
3'52"
Pan American Health Organization

Kesho isiyo na saratani ya shingo ya kizazi kwa Wanawake Tanzania

Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni kanda ya Afrika linaeleza kuwa Saratani ya shingo ya kizazi ni moja ya sababu kuu za vifo vinavyotokana na saratani kwa wanawake nchini Tanzania. Kawaida saratani ya shingo ya kizazi huathiri wanawake wenye zaidi ya umri wa miaka 25 ambao wameambukizwa virusi vya papilloma ya binadamu na hawajapata chanjo. Makala hii iliyoandaliwa na WHO na kusimuliwa na Anold Kayanda inaeleza jinsi uchunguzi wa afya wa mara kwa mara ni njia nzuri ya kuzuia saratani ya shingo ya kizazi..  
 

Sauti
3'23"