Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WD2023 imeonesha kuwa wanawake tunachukua hatua mashinani - Martha Wanza

WD2023 imeonesha kuwa wanawake tunachukua hatua mashinani - Martha Wanza

Pakua

Mkutano wa kimataifa wa Women Deliver 2023 (WD2023) au wanawake wanatekeleza umekunja jamvi mwishoni mwa wiki mjini Kigali nchini Rwanda baada ya kuwaleta pamoja washiriki 6,000 ana kwa ana na wengine zaidi ya 200,000 mtandaoni. Lengo kuu la mkutano huo mkubwa kabisa uliozanza Julai 17 hadi 20 na kubeba kaulimbiu “Nafasi, mshikamano na suluhu” lilijikita katika ujumuishwaji ili kusongesha usawa endelevu wa kijinsia kwa kuhusisha sekta mbalimbali. Wadau wakiwemo wakuu wa nchi na serikali na mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo linalohusika na masuala ya wanawake UN-Women na la idadi ya watu na afya ya uzazi UNFPA walikuwa mstari wa mbele katika mkutano huo Martha Wanza alikuwa miongoni mwa washiriki kutoka Kenya , anafanyakazi na shirika lijulikanalo kama Jumuiya ya wanawake vijana Wakristo nchini humo YWCA. Amezungumza na Eugene Uwimana Afisa uratibu msaidizi wa maendeleo, mawasiliano na mipango katika ofisi ya Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa  nchini Rwanda , maswali yake ynarejewa studio na Flora Nducha na Martha akianza kwa kumfafanulia kuhusu shirika lao

Audio Credit
Anold Kayanda/Flora Nducha
Audio Duration
4'8"
Photo Credit
UN/Eugene Uwimana