Mkimbizi aliyerejea nyumbani Burundi kutoka Tanzania awaambia wenzake, "rejeeni nyumbani tujenge nchi yetu."
Akiwa katika ziara yake ya kwanza nchini Burundi hivi karibuni, Naibu Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi duniani, UNHCR Kelly Clements ameihi jamii ya kimataifa iongeze msaada kwa maeneo na jamii ambako wakimbizi wa Burundi wameamua kurejea nyumbani kwa hiari.
Tangu mwaka 2017, zaidi ya wakimbizi 200,000 wa Burundi wamerejea nyumbani kutoka nchi jirani kama vile Tanzania.