Serikali ya Tanzania itakomboa watu wenye ulemavu kwa kuboresha mfumo wa ajira serikalini - Shega Mboya
Serikali nchini Tanzania imeshauriwa kuboresha Sekretarieti ya mfumo wa uombaji ajira kwa njia ya mtandao maarufu kama Ajira Portal ili uweze kuwatambua watu wenye ulemavu na hivyo kumiza matakwa ya sera ya ajira ambayo ina kipengele mahususi kinacholenga kuwajumuisha watu wenye ulemavu. Ushauri huo umetolewa na Shega Mboya wa Morogoro, Tanzania ambaye pamoja na kuwa na elimu ya juu ya digrii mbili, hajaweza kupata ajira ingawa anaamini pamoja na vigezo vingine ambavyo anaamini anavyo, laiti mfumo wa kidijitali ungeweza kutambua watu wenye ulemavu, ingekuwa rahisi kwake na kwa we