Umoja wa Mataifa waendelea kutoa misaada ya dharura Madagascar
Kwa kipindi cha mwezi mmoja tu, nchi ya Madagascar imekabiliana na vimbunga vinne. Jumanne iliyopita, kimbunga Emnati kiliathiri maeno yaleyale yaliyoathirika na kimbunga Batsirai na kuwafurusha makwao maelfu ya watu. Umoja wa Mataifa unashirikiana na wadau wa kibinadamu na serikali ya Madagascar kuwasaidia wale wanaohitaji misaada ya dharura.