Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Harakati za Benki ya Dunia kuuboresha mji wa Libiąż, Poland dhidi ya makaa ya mawe

Harakati za Benki ya Dunia kuuboresha mji wa Libiąż, Poland dhidi ya makaa ya mawe

Pakua

Kuondoa makaa ya mawe ni mojawapo ya hatua muhimu zaidi za kupambana na mabadiliko ya tabianchi na kulinda sayari. Kuhama kutoka katika matumizi ya makaa ya mawe hadi nishati safi hupatia jamii fursa muhimu za kiuchumi na kijamii pia. Mji wa Libiąż, Poland, ulio katika eneo la uchimbaji wa makaa ya mawe ambao umedumu kwa karne nyingi, uko katikati ya mabadiliko haya. Serikali za mitaa, vikundi vya jamii, vyama vya wafanyakazi, na mashirika ya kiraia yanafanya kazi pamoja ili kunufaisha uchumi wa ndani, kurejesha ardhi ya zamani ya uchimbaji madini, na kutoa mafunzo kwa wafanyakazi kwa ajili ya kazi za kijani au kazi zisizoharibu mazingira. Benki ya Dunia inashirikiana na mataifa mbalimbali wazalishaji wa makaa ya mawe kote duniani, kuondokana na nishati hii hatari kwa mazingira na sayari dunia kwa ujumla.

Audio Credit
Assumpta Massoi/Anold Kayanda
Audio Duration
3'27"
Photo Credit
© Unsplash/Jose Chinchilla