Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Haki za watu wenye ualbino Uganda, sasa zatambulika kisheria, waliowabagua watozwa fedha

Haki za watu wenye ualbino Uganda, sasa zatambulika kisheria, waliowabagua watozwa fedha

Pakua

Watu wenye ualbino wamekuwa wakikumbwa na changamoto lukuki ikiwemo za kijamii, kiafya na kiuchumi hali inayofanya mustakabali wao kuwa na mashaka na hata wakati mwingine wanakuwa na wasiwasi kuhusu ndoto zao . Lakini kwa mtoto Elizabeth Ayebare ambaye ndoto yake ilikuwa almanusura itumbukie shimoni, mambo sasa ni shwari kwani sheria ilifuata mkondo wake na waliokuwa wanataka kupeperusha ndoto yake wakachukuliwa hatua ya kumlipa fidia na sasa anaendelea na masomo yake kama kawaida. Nini kilifanyika? Simulizi nzima anayo Anold Kayanda katika Makala hii iliyoandaliwa na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu.

Audio Credit
Leah Mushi/Anold Kayanda
Audio Duration
4'35"
Photo Credit
OHCHR Video