Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanaharakati huko COP27 wasema hakuna hatua kwa tabianchi bila kujali haki za binadamu

Wanaharakati huko COP27 wasema hakuna hatua kwa tabianchi bila kujali haki za binadamu

Pakua

Huko Sharm-el-Sheikh nchini Misri, kwenye mkutano wa 27 wa nchi wanachama wa Mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP27, tarehe 17 mwezi huu wa Novemba yalishuhudiwa maandamano ya maelfu ya wawakilishi wa watu wa jamii ya asili, wanawake, wanarahakati wa masuala ya jinsia, vijana, mazingira na haki kwa tabianchi kutoka pande mbalimbali za dunia. Wao waliandamana kwa niaba ya maelfu ya mashirika na mamilioni ya watu  na kupitisho azimio lao la umma kuhusu haki kwa tabianchi. Wanapaza sauti je ni sauti zipi? Wanataka nini? Anold Kayanda amefuatilia maandamano hayo na kuandaa Makala haya..

Audio Credit
Flora Nducha/Assumpta Massoi
Audio Duration
3'51"
Photo Credit
Laura Quinones