Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana wa Afrika wataka hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi zichukuliwe haraka

Vijana wa Afrika wataka hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi zichukuliwe haraka

Pakua

Ule usemi wa vijana ni taifa la kesho, umeonekana kuwa kesho haitaweza kufika na ndio maana vijana kutoka kila pembe ya dunia wamefunga safari kwenda kuhudhuria mkutano wa 27 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP27 unaofanyika huko nchini Misri. 

Vijana hao wake kwa waume wamefanya mambo mbalimbali ikiwemo kushiriki katika mikutano ya wakuu wa nchi na serikali, kufanya maandamano nje ya kumbi za mikutano na pia kuendesha mikutano wenyewe kueleza kile wanachotaka kifanyike na tena kwa kuwashirikisha ili dunia kukabiliana na changamoto zinazoletwa na mabadiliko ya tabianchi.Wanasema hawataki tena 'Bla Bla'. Tuungane na Leah Mushi aliyefuatilia na kuandaa makala ifuatayo.

Audio Credit
Selina Jerobon/Leah Mushi
Sauti
3'29"
Photo Credit
UN News/Laura Quinones