Maji ni uhai na yanabadili maisha ya watu na jamii zao:UNCDF
Mradi wa nishati ya maji wa AHEPO upo katika kijiji cha Lifakara kwenye maporomoko ya Mbangamao kwenye mto Mtandasi wilayani Mbinga mkoani , Ruvuma Kusini mwa Tanzania.
Mradi huo ambao unafadhiliwa na shirika la mitaji la Umoja wa Mataifa UNCDF unalenga sio tu kuwapunguzia adha wananchi wa wilaya hiyo bali pia kubadili kabisha maisha yao ya kiuchumia na kijamii kwa kuwapata nishati mbadala kwani fursa ya nishati ni kitovu cha maendeleo ya jamii yoyote na ni moja ya mambo ya lazima katika kukidhi mahitaji muhimu na ya msingi ya binadamu.