Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukame Kenya: Serikali imeanza mchakato wa kufadhili Mfuko wa Taifa wa Dharura lakini tunahitaji usaidizi kuokoa maisha ya watu

Ukame Kenya: Serikali imeanza mchakato wa kufadhili Mfuko wa Taifa wa Dharura lakini tunahitaji usaidizi kuokoa maisha ya watu

Pakua

Umoja wa Mataifa na wadau wake wa masuala ya kibinadamu nchini Kenya wameomba dola milioni 472.6 kusaidia watu milioni 4.3 walioathiriwa na ukame, ili kuunga mkono mwitikio unaoongozwa na Serikali, huku janga hilo likitarajiwa kuwa mbaya zaidi. Hali katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo katika Pembe ya Afrika, ni mbaya. Naibu Rais wa Kenya Rigathi Gachagua anaeleza kuwa mzigo huu wa janga la mabadiliko ya tabianchi ni mkubwa kwa nchi yake na kwa hivyo ni muhimu jumuiya ya kimataifa ikasaidia lengo hilo la Umoja wa Mataifa kwani hali ya wananchi inazidi kuwa mbaya. Mfano mmoja ni katika Kaunti ya Garissa ambako video iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa Mazingira, UNEP, inaonesha hali ya wananchi kuwa maisha yako hatarini. Kutoka Kenya, Mwadishi wetu Thelma Mwadzaya anaeleza zaidi kupitia makala hii.  

Audio Credit
Anold Kayanda/Thelma Mwadzaya
Audio Duration
5'6"
Photo Credit
© UNICEF/Lamek Orina