Msaada kutoka FAO waleta matumaini kwa wakazi wa Hirshabelle nchini Somalia
Pakua
Ukame wa zaidi ya miongo minne na mafuriko vimekuwa ‘mwiba’ kwa wananchi wa Somalia na hivyo kutishia uhakika wa kupata chakula halikadhalika mbinu za kujipatia kipato. Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO kwa msaada kutoka serikali ya Sweden imewezesha mradi wa kusaidia wakulima wadogo kwa kuwapatia pembejeo na msaada wa fedha na sasa kuna nafuu hasa kwenye jimbo la Hirshabelle nchini humo.
Mradi huo uko kwenye maeneo ya Johwar na Beledweyne na manufaa yameanza kuonekana huku wakulima wakilinganisha kabla na baada ya kupata usaidizi. Kwa kina basi kuhusu kilichofanyika ungana na Thelma Mwadzaya kwenye Makala hii iliyofanikishwa na FAO.
Audio Credit
Selina Jerobon/Thelmwa Mwadzaya
Audio Duration
4'6"