Wengi wetu hatukamilishi makundi yote matano ya chakula-Afisa Lishe Mwanjisi.
Emmanuel Mwanjisi ni Afisa lishe kutoka hospitali ya Consolatha, Ikonda, katika wilaya ya Makete, nyada za juu kusini mwa Tanzania, anaeleza faida za ulaji wa mbogamboga na matunda katika mwili wa binadamu ikiwemo kuimarisha kinga za mwili.
Bwana Emmanuel anaeleza kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakila milo ambayo haizingatii makundi matano ya chakula, na mara nyingi makundi ya mbogambona na matunda ndio yanayoondolewa katika mpangilio wa vyakula na matokeo yake kutetereka kwa afya za wanadamu.