Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakulima wa mboga za majani na matunda wainua kipato chao Tabora nchini Tanzania

Wakulima wa mboga za majani na matunda wainua kipato chao Tabora nchini Tanzania

Pakua

Katika kuendelea na mfululizo wa makala kuhusu mwaka wa kimataifa wa mboga mboga na matunda, IYFV leo tunarejea tena mkoani Tabora nchini Tanzania kumulika ni kwa vipi wakazi wa mkoa huo wanatumia kilimo mboga mboga na matunda kama njia siyo tu ya kujipatia lishe bora bali pia kuinua kipato cha familia na kugharimia matumizi ya nyumbani. Hii ni katika kuthibitisha kile ambacho Umoja wa Mataifa unasema kuwa mboga mboga na matunda vinaweza kuwa suluhu la umaskini na njaa duniani iwapo wakazi wa dunia hii watatambua jinsi ya kulima vyema na kuongeza thamani ya mazao hayo. Mwenyeji wetu mkoani Tabora ni Diana Katabarwa wa radio washirika Radio Uhai FM. 

Audio Credit
Flora Nducha/Diana Katabarwa
Audio Duration
4'25"
Photo Credit
UNICEF/Giacomo Pirozzi