Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wengi wetu hatukamilishi makundi yote matano ya chakula-Afisa Lishe Mwanjisi.

Wengi wetu hatukamilishi makundi yote matano ya chakula-Afisa Lishe Mwanjisi.

Pakua

Emmanuel Mwanjisi ni Afisa lishe kutoka hospitali ya Consolatha, Ikonda, katika wilaya ya Makete, nyada za juu kusini mwa Tanzania, anaeleza faida za ulaji wa mbogamboga na matunda katika mwili wa binadamu ikiwemo kuimarisha kinga za mwili. 

Bwana Emmanuel anaeleza kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakila milo ambayo haizingatii makundi matano ya chakula, na mara nyingi makundi ya mbogambona na matunda ndio yanayoondolewa katika mpangilio wa vyakula na matokeo yake kutetereka kwa afya za wanadamu. 

Mtaalamu huyo anaungana na Umoja wa Mataifa katika mwaka huu wa 2021 uliopitishwa kuwa mwaka wa mbogamboga na matunda ili kuhamasisha watu kuzingatia ulaji wa mbogamboga na matunda kwa ajili ya afya zao n ahata kuwa chanzo cha kipato. Katika sehemu hii ya kwanza, mtaalamu huyo anazungumzia mmbogamboga.  

Audio Credit
Assumpta Massoi/Zawadi Kikoti
Photo Credit
© FAO-Magnum Photos/Alex Webb