Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunatumia muarobaini kuzuia wadudu waharibifu wa mboga za majani- Bi. Kibasa

Tunatumia muarobaini kuzuia wadudu waharibifu wa mboga za majani- Bi. Kibasa

Pakua

Katika mwaka huu wa mboga za majani na matunda, Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la chakula na kilimo, FAO, unataka utumike kama njia ya kuibua fursa mpya za kuendeleza lishe na kipato kupitia vyakula hivyo. Mathalani maeneo ya mijini, FAO inasema mbinu bora zinaweza kupatia fursa wakazi kulima mboga za majani na hata matunda na kuuza au hata wao kula wenyewe na kuimarisha afya na kipato. Afya huanzia shambani na hivyo matumizi ya mbolea sahihi ni jambo la msingi. Hivyo ndivyo imekuwa kwa Mary Kibasa na wenzake huko jijini Dar es salaam, ambako wanalima mboga eneo la Kinondoni, katikati ya wakazi huku wakizingatia afya siyo tu za kwao bali za walaji. Ahimidiwe Olotu wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa, UNIC jijini Dar es salaam, anaendelea na mazungumzo yake na Mary akiwa shambani kwake na katika hii sehemu ya pili na ya mwisho anaezea changamoto na mbolea watumiazo.

Audio Credit
ANOLD KAYANDA/ AHIMIDIWE
Photo Credit
UN Tanzania/Ahimidiwe Olotu