Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kilimo cha mjini ndio mwendo wa sasa- Bi. Kibasa 

Kilimo cha mjini ndio mwendo wa sasa- Bi. Kibasa 

Pakua

Katika mwaka huu wa mboga za majani na matunda, Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la chakula na kilimo, FAO, unataka utumike kama njia ya kuibua fursa mpya za kuendeleza lishe na kipato kupitia vyakula hivyo. Mathalani maeneo ya mijini, FAO inasema mbinu bora zinaweza kupatia fursa wakazi kulima mboga za majani na hata matunda na kuuza au hata wao kula wenyewe na kuimarisha afya na kipato. Hivyo ndivyo imekuwa kwa Mary Kibasa na wenzake huko jijini Dar es salaam, ambako wanalima mboga eneo la Kinondoni, katikati ya wakazi huku wakizingatia afya siyo tu za kwao bali za walaji. Je nini kinafanyika? Ahimidiwe Olotu wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa, UNIC jijini Dar es salaam, amemtembelea Mary akiwa shambani kwake na kuzungumza naye katika hii sehemu ya kwanza ambapo sehemu ya pili itakujia kesho. 

Audio Credit
Assumpta Massoi/Ahimidiwe Olotu
Audio Duration
4'23"
Photo Credit
UN Tanzania/Ahimidiwe Olotu