Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi na changamoto ya kupata matunda na mboga Uganda.

Wakimbizi na changamoto ya kupata matunda na mboga Uganda.

Pakua

Jamii ya wakimbizi ni miongoni mwa jamii zilizo hatarini kukabiliwa na utapiamlo kutokana na kutokuwa na mazingira bora ya kushiriki kwenye kilimo hasa upanzi wa mbogamboga na matunda. Pia kutokana na hali ya utegemezi wa msaada wa kibinadamu, wengi wao huwa hawana uwezo wa kununua matunda haya au mbogamboga. Licha ya changamoto hizo, juhudi zimekuwa zikifanywa ambazo zimeleta nuru hasa kwa kuwafundisha wakimbizi kutumia mbinu bunifu kupanda mbogamboga majumbani kwao. 

Je, wanafanyaje? Basi ungana na John Kibego akimhoji mkimbizi Racheal Wase kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC anayeishi katika kambi ya wakaimbizi ya Kyangwali.  

Audio Credit
Anold Kayanda/John Kibego
Audio Duration
3'40"
Photo Credit
UNICEF/Giacomo Pirozzi