Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunatumia Sombe (Kisamvu) ili mama mzazi apate maziwa- Scovia 

Tunatumia Sombe (Kisamvu) ili mama mzazi apate maziwa- Scovia 

Pakua

Makala hii ni sehemu ya pili ya mahojiano kati ya mwandishi wa UN News Kiswahili nchini Uganda John Kibego wa Uganda na Scovia Atuhura Habimana, mkazi wa Uganda, mkimbizi kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC. Katika sehemu ya kwanza Scovia alianza kueleza umuhimu wa aina mbalimbali za mboga za majani na matunda kwa wasichana na wanawake. Leo Scovia ambaye ameolewa nchini Uganda katika jiji la Hoima anaendelea kueleza umhimu huo akijikita na mboga aina ya sombe au kisamvu hususani kwa mama na mtoto wakati huu ambapo tunaendelea kumulika faida za mbogamboga na matunda kwa kutambua mwaka wa kimataifa wa mboga na matunda uliotangazwa na Umoja wa Mataifa.  Ungana nao katika sehemu hii ya pili.

Audio Credit
Assumpta Massoi/John Kibego
Audio Duration
3'38"
Photo Credit
UN/ John Kibego