Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ulaji wa mbogamboga na matunda siyo suala la kipato, ni uelewa. 

Ulaji wa mbogamboga na matunda siyo suala la kipato, ni uelewa. 

Pakua

Mkoa wa Njombe, ni miongoni mwa mikoa iliyoko nyanda za juu kusini mwa Tanzania. Eneo hili linatajwa kuwa lenye rutuba ambalo lina mazingira mazuri ya kuweza kustawisha mbogamboga na matunda ya aina mbalimbali kama vile matufaa, parachichi na mengine mengi. Laicha ya hali hiyo, mkoa huu ni miongoni mwa maeneo yenye watu wenye utapiamlo, ukitajwa kuwa na asilimia 53.6 ya watu wake wenye utapiamlo.  

Kwa kutambua hali kama hiyo katika maeneo mengine ulimwenguni, Umoja wa Mataifa umeutangaza mwaka huu  wa 2021  kuwa wa mbogamboga na matunda,  (IYVF)  lengo likiwa ni kuelimisha watu kuhusu umuhimu na faida za mbogamboga na matunda.  

Kutoka wilaya ya Makete, mkoani Njombe Tanzania, Zawadi Kikoti wa redio washirika Green anazungumza na baadhi ya wananchi kuhusu uelewa wao katika ulaji wa mbogamboga na matunda. Kwanza ni Subira Mbilinyi. 

Audio Credit
Assumpta Massoi/Zawadi Kikoti
Audio Duration
4'2"
Photo Credit
© FAO/Miguel Schincariol