Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

UNDP Tanzania/Sawiche Wamunza

UNDP yapiga jeki juhudi za wakulima wa pilipili Tanzania

Nchini Tanzania harakati za kuondokana na umaskini zinaendelea kushika kasi mashinani zikipigiwa chepuo na Umoja wa Mataifa. Miongoni mwa hatua hizo ni kilimo cha kisasa cha mboga mboga na matunda kinachoendeshwa na wanawake kupitia chama cha wakulima wa mboga na matunda nchini Tanzania, TAHA. TAHA imepatiwa msaada na shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP nchini Tanzania na sasa kupitia vikundi mbalimbali, wakulima wanalima mazao ambayo yanakidhi vigezo vya kuuzwa nje ya nchi.

Sauti
5'38"
UN-Habitat/Julius Mwelu

Tunafanikiwa kuwaelimisha watu wasichafue mazingira wakati wa msimu wa mvua-Jikomboe Youth Group

Katika miji mikubwa nchini Tanzania, msimu wa mvua ni msimu unaokuja na changamoto kadha zikiwemo za magonjwa, mafuriko na uchafuzi wa mazingira kutokana na watu kutumia mwanya huo kutupa taka kwa kutegemea maji ya mvua kuzibeba taka hizo. Ni bahati mbaya kuwa baadhi ya taka hizo kama plastiki huishia katika mazingira au vyanzo vya maji na mifereji na kusababisha matatizo kwa mazingira.
Sauti
3'53"
UN News Kiswahili

Kupata utambuzi na tuzo maana yake kazi yako imeonekana na ni fursa kufanya zaidi

Shirika lisilo la kiserikali la CAMFED nchini Tanzania ni moja ya mashirika yanayopambana kuhakikisha yanachangia katika kutimiza angalau malengo machache kati ya malengo 17 ya maendeleo endelevu, SDGs. Shirika hili kwa kiasi kikubwa limejikita katika lengo namba 4 linalozungumzia elimu bora na lengo namba 5 linazungumzia usawa wa kijinsia, yote hayo yakiwa yanalenga kutomwacha nyuma mtu yeyote katika maendeleo ya ulimwengu ifikapo mwaka 2030. 

Sauti
4'1"
UN News/ John Kibego

Kijana mkimbizi kutoka Sudan Kusini atuzwa kwa kusoma habari za Kingereza Uganda

Licha ya changamoto za ukimbizini hasa wakati huu wa COVID-1, bado kuna mianya ya tabasamu kwa vijana wakimbizi wanojitahidi kushiriki kwenye fursa chache zilizopo.

Nchini Uganda katika mji wa Hoima, kijana mkimbizi, Emmanuel Edema kutoka Sudan Kusini ametuzwa baada ya kuibuka msomaji bora wa habari za lugha ya Kingereza  kwenye mashindano yalioandaliwa na redio washirika Spice FM.

Sauti
3'42"
UN Environment/Georgina Smith

Wanawake Tanga hatujibweteki, tunajishughulisha

Wanawake 10 mkoani Tanga Tanzania wameunda kikundi cha kushirikiana kufanya shughuli mbalimbali za kujiingizia kipato ambapo wanatumia zao la mkonge au katani kutengeneza bidhaa mbalimbali, shughuli ambayo imewainua kiuchumi. Stella Vuzo wa Kituo cha habari za Umoja wa Mataifa, UNIC Dar es Salaam akiwa mkoani Tanga Tanzania amezungumza na mmoja wa wanawake hao. 

Sauti
3'25"
UNEP GRID Arendal/Peter Prokosch

Tunapowalinda wanyama, tunajilinda wenyewe-Jim Justus Nyamu

Wanyamapori wamekuwa  ni kitenga uchumi kwa nchi nyingi za Afrika lakini sekta hii inakumbwa na changamoto za kila siku zikiwemo uwindaji haramu wa wanyama pori wakati ndovu wakiwa miongoni mwa wanyama wanaowindwa zaidi kutokana na thamani ya pembe zake.

Jim Justus Nyamu kutoka nchini Kenya, mwaka 2012 alinzisha kampeni ya kuhamasisha kuhusu umuhimu wa kuwalinda ndovu mwaka 2012, na amefanya ziara katika nchi mbalimbali duniani kufanya shughuli hiyo.

Mwandishi wetu wa Kenya Jason Nyakundi amezungumza na Bwana Nyamu.

Sauti
3'32"
World Bank/Simone D. McCourtie

Teknolojia ya dijitali imetupa suluhisho la mambo mengi-Vijana Kenya

Teknolojia ya dijitali imeleta  mabadiliko makubwa na ya haraka duniani;  uchumi, mawasiliano,  elimu na nyingine nyingi. Teknolojia ni moja ya ajenda zinazozungumziwa kwenye mkutano mkuu wa 75 wa Baraza la Umoja wa Mataifa. Asilimia kubwa ya watumiaji wa teknolojia ya dijitali ni vijana ambao wana muda wa kutosha kuitumia katika mambo tofauti. Mwandishi wa Nairobi Jason Nyakundi amezungumza  na vijana kuhusu ni kwa njia zipi wanaitumia teknolojia.

Sauti
3'25"
UN Kenya/Newton Kanhema

COVID-19 ilitukuta bila kujiandaa, lakini tumejifunza-Wananchi Kenya

Maadhimisho  ya miaka 75 wa Umoja wa Mataifa yanafanyika wakati dunia inakabiliwa na janga baya zaidi kuwahi kushuhudiwa kwa miaka mingi, virusi vya corona. Vifo pamoja na hasara nyingine kama kupoteza kazi na biashara, vimerudisha nyuma maendeleo yaliyofikiwa kwa miongo mingi.  Lakini watu wameweza kujifunza nini hasa kutokana na janga hili la virusi vya corona? Mwandishi wetu wa Kenya Jason Nyakundi amezungumza na baadhi ya wananchi wa Kenya. 

Sauti
3'18"