Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

World Bank / Sarah Farhat

Watoto wa kike Morogoro Tanzania wameitaka jamii kuacha vitendo vya kikatili dhidi yao

Dunia ikiwa katika mfululizo wa siku 16 za kuahamasisha mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia, nchini Tanzania mkoani Morogoro wasichana wamepaza sauti wakionesha kutofurahishwa na ukatili unaofanywa na baadhi ya wazazi na walezi majumbani. Huku wakiiomba serikali kufuata sheria pale mtuhumiwa anapo kamatwa na kufikishwa mahakamani, kwa makosa ya ukatili dhidi ya watoto wa kike. 

Sauti
3'21"
UN Tanzania/Ahimidiwe Olotu

Wanaume waliona utamu wa kuongoza, wakawaacha dada zao-Getrude Mongela

Ulimwengu ukiwa katika siku 16 za uhamasishaji wa kupinga ukatili dhidi ya wanawake, pamoja na mengine, jamii inakumbushwa kuhusu lengo namba 5 la malengo ya Umoja wa Mataifa ya maendelepo endelevu, SDGs, lengo ambalo linahamasisha kuhusu usawa wa kijinsia. Lakini jamii za ulimwengu zilifikaje katika kuwa na pengo la usawa wa kijinsia kwa kiasi hiki cha kuwa na uhitaji wa kukumbushwa? Bi.

Sauti
3'21"
UNMISS\Nektarios Markogiannis

Wakati mwingine watu wanafanyiwa vitendo vya ukatili lakini hawajui kuwa huo ni ukatili- Mary Nsia Mangu 

Msichana Mary Nsia Mangu wa Arusha Tanzania, ili kuunga mkono Malengo ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo endelevu, SDGs, anaendesha taasisi maalum ya Dexterous Tanzania ambayo ina lengo la kuboresha elimu ya watoto, kuwapatia uelewa kupitia vitabu na pia kuwafahamisha kuhusu ukatili wa kijinsia.  

Vile vile taasisi yake inasaidia kupinga ukatili dhidi ya watoto hususani wa Kike kwa kuwapa elimu kupitia njia mbalimbali ikiwamo kuwafikia moja kwa moja shuleni. Mary anawahamasisha wasichana kuwa majasiri kuleta mabadiliko ndani ya Jamii. 

 

Sauti
2'53"
UN News/ John Kibego

Wazee wazungumza historia ya mafuriko kwenye Ziwa Albert

Maelfu ya watu wanendelea kuathiriwa na mafuriko yanayoshuhudiwa katikaa meneo mbalimbali hasa yale ya Ziwani nchini Uganda.

Licha ya onyo kutoka kwa serikali na asasi za kiraia kuwa mafuriko haya yanaweza kuendelea, mpaka sasa baadhi ya watu wanahama mita chache wakiwa na matumaini kwamba maji haya yatapungua mambo yarejee kama kawaida.

Hata hivyo, watu wa asili kwenye Ziwa Albert wanaonya kuwa mambo bado kutokana na mfano kama huo ulioshuhudiwa na waliokuwepo miaka ya elfu moja kendamia sitini.

Sauti
3'58"
Picha ya maktaba ya UM

Tulianzisha shirika la mazingira ili kupambana na uchafu na ukosefu wa ajira-Sam Dindi  

Ikiwa leo ni siku ya choo duniani, Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO, linaeleza kuwa Ulimwenguni, asilimia 80 ya maji taka yanayozalishwa na jamii yanarudi katika mzunguko wa ikolojia bila kusafishwa,  na vilevile taka mwili za binadamu zisizodhibitiwa mathalani kwa kuwekewa dawa za kuua vijidudu, huingia kwenye mazingira na kueneza magonjwa hatari na sugu.   

Sauti
4'31"
ILO/Video Capture

Taka za mferejini Haiti zageuzwa kazi za sanaa na kuibua vipaji vya vijana waliokata tamaa.

Kitongoji cha Cité Soleil, kwenye mji mkuu wa Haiti, Port au Prince, unatambulika kwa maisha duni, umaskini uliokithiri na ghasia za kila uchao. Vijana wamekata tamaa! Lakini Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la kazi duniani, ILO limeona hali hiyo haiendani sawa na ajenda yake ya 2030 ya kutomwacha yeyote nyuma. Hivyo ilianzisha mradi wa kuibua vipaji vya vijana kupitia kazi za kusafisha mfereji uliokuwa umejaa taka na kuchafua mazingira ya mji huo. Je nini kimefanyika? Na vijana wananufaika vipi hadi kuona tena nuru katika maisha yao?

Sauti
3'42"
Doris Mollel Foundation.

Mtoto kuzaliwa njiti si mkosi, akipatiwa matunzo anakua- Doris Mollel

Kila mwaka takribani watoto milioni 15 wanazaliwa njiti, yaani ujauzito ukiwa haujatimiza wiki 37. Takwimu hizo ni kwa mujibu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO ambalo linasema kuwa idadi inaongezeka. Kuzaliwa njiti ni moja ya sababu ya vifo vya watoto wenye umri wa chini ya miaka 5 na leo katika kuadhimisha siku ya kuhamasisha umma kuhusu watoto njiti, wito unatolewa ili kusaidia zaidi watoto hao. Taasisi ya Doris Mollel nchini Tanzania imejikita katika kusaidia watoto njiti kwa kuzingatia kuwa Mkurugenzi Mtendaji mwenyewe Doris alizaliwa njiti akiwa na uzito wa gramu 900.

Audio Duration
5'28"
UN News/ John Kibego

Wanahabari wahaha kutetea mazingira licha ya changamoto

Uhifadhi wa mazingira ni miongoni mwa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) ikiwa ni nguzo ya kudhibiti madhara ya mabadiliko ya tabianchi ambalo linachagiza mataifa kutunza na kukuza utunzaji wa mazingira.

Lakini kutokana na ukweli kwamba mazingira yanahifadhi rasilimali zinazotakiwa kutekeleza maendeleo, vuta nikuvute imeshuhudiwa kwenye nchi nyingi juu ya rasilimali za misitu na mali nyingine katika maeneo nyeti ikmazingira.

Sauti
2'54"
UN News/ John Kibego

Mikopo ya bodaboda yageuka kaa la moto kutokana na COVID-19 Uganda

Nchini Uganda, serikali ilipatia vijana mikopo ili kuwawezesha kujinasua kiuchumi na hivyo kuwa sehemu ya utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Hata hivyo mafuriko katika Ziwa Albert na mlipuko wa ugonjwa wa Corona, COVID-19 vimevuruga uwezo wa vijana kurejesha mkopo huo. Sasa vijana kupitia vyongozi wao wanaomba serikali kutotumia mkono wa sheria dhidi ya wanaopata matatizo kuzingiatia ratiba ya ulipaji wa fedha walizopatiwa.

Sauti
3'40"