Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

UNEP GRID Arendal/Peter Prokosch

Tunapowalinda wanyama, tunajilinda wenyewe-Jim Justus Nyamu

Wanyamapori wamekuwa  ni kitenga uchumi kwa nchi nyingi za Afrika lakini sekta hii inakumbwa na changamoto za kila siku zikiwemo uwindaji haramu wa wanyama pori wakati ndovu wakiwa miongoni mwa wanyama wanaowindwa zaidi kutokana na thamani ya pembe zake.

Jim Justus Nyamu kutoka nchini Kenya, mwaka 2012 alinzisha kampeni ya kuhamasisha kuhusu umuhimu wa kuwalinda ndovu mwaka 2012, na amefanya ziara katika nchi mbalimbali duniani kufanya shughuli hiyo.

Mwandishi wetu wa Kenya Jason Nyakundi amezungumza na Bwana Nyamu.

Sauti
3'32"
World Bank/Simone D. McCourtie

Teknolojia ya dijitali imetupa suluhisho la mambo mengi-Vijana Kenya

Teknolojia ya dijitali imeleta  mabadiliko makubwa na ya haraka duniani;  uchumi, mawasiliano,  elimu na nyingine nyingi. Teknolojia ni moja ya ajenda zinazozungumziwa kwenye mkutano mkuu wa 75 wa Baraza la Umoja wa Mataifa. Asilimia kubwa ya watumiaji wa teknolojia ya dijitali ni vijana ambao wana muda wa kutosha kuitumia katika mambo tofauti. Mwandishi wa Nairobi Jason Nyakundi amezungumza  na vijana kuhusu ni kwa njia zipi wanaitumia teknolojia.

Sauti
3'25"
UN Kenya/Newton Kanhema

COVID-19 ilitukuta bila kujiandaa, lakini tumejifunza-Wananchi Kenya

Maadhimisho  ya miaka 75 wa Umoja wa Mataifa yanafanyika wakati dunia inakabiliwa na janga baya zaidi kuwahi kushuhudiwa kwa miaka mingi, virusi vya corona. Vifo pamoja na hasara nyingine kama kupoteza kazi na biashara, vimerudisha nyuma maendeleo yaliyofikiwa kwa miongo mingi.  Lakini watu wameweza kujifunza nini hasa kutokana na janga hili la virusi vya corona? Mwandishi wetu wa Kenya Jason Nyakundi amezungumza na baadhi ya wananchi wa Kenya. 

Sauti
3'18"
UN News/ John Kibego

Wakimbizi watoa maoni kuhusu kazi za Umoja wa Mataifa, Uganda

Umoja wa Mataifa ambao umetimiza miaka 75 tangu kuanzishwa kwake, unaendelea kufanya  mengi kuboresha maisha ya watu katika vikundi mbalimbali vya jamii na serikali ili kuboresha maisha yao, kuchochea maendeleo na vilevile kuhakikisha utulivu katika maeneo yenye migogoro.

Umoja huo una maana kubwa kwa jamii za wakimbizi hasa kupitia shirika lake la kuhudumia wakimbizi, UNHCR. Je, mchango wake miongoni mwa wakimbizi unathaminiwa?

Sauti
3'35"
World Bank/Maria Fleischmann

Kutoa ni moyo si utajiri

Bi Neema Mustafa mkazi wa Kijiji cha Kiswanya, wilayani Kilombero, Morogoro Tanzania ni mtu mwenye ulemavu ambaye anaishi katika hali ya kupooza kwa zaidi ya miaka 20 tangu  alipopooza mwili wake akiwa na msichana mdogo wa umri wa takribani miaka 20. Neema aliamua kumsaidia mtoto Omar ambaye alikuwa katika hali mbaya ya utapiamlo uliosababisha udumavu baada ya changamoto za maisha ya wazazi wa mtoto huyo kuwafanya washindwe kumlea.

Audio Duration
4'15"
UN Kenya/Newton Kanhema

COVID-19 imenirudisha nyumbani kijijini-Waweru

Tangu lizuke janga la corona duniani athari nyingi za karibu kila sekta zimeshuhudiwa. Vijana ambao idadi yao ndiyo kubwa kwa karibu kila nchini duniani nao wameathirika pakubwa. Wengi walilazimika kusitisha masomo kufuatia kufungwa shule na taasisi za elimu, wengine wakapoteza ajira na kubaki katika hali ya sintofahamu kuhusu hatma ya maisha yao. Kijana Joseph Waweru alipoteza kibarua chake mjini Nairobi na pia mipango yake ya masomo katika chuo kikuu ikakwama ndipo akaamua kuhamia kwao alikozaliwa huko Kitale, magharibi mwa Kenya.

Sauti
3'35"
© ITU/M. Jacobson – Gonzalez

Apps and Girls, taasisi iliyodhamiria kuwainua wasichana katika TEHAMA nchini Tanzania

Ni ukweli ulio wazi kwamba duniani kote bado kuna pengo kubwa la wasichana katika teknolojia ya mawasiliano yaani TEHAMA ingawa juhudi za hivi karibuni, kimataifa na kitaifa zinaonesha kuanza kuzaa matunda kwani wasichana wanazidi kushawishika kuingia katika masomo yanayohusisha TEHAMA. Mafaniko ya juu ni vigumu kuyafikia ikiwa jamii kwa ujumla kuanzia mtu mmojammoja hatahusika katika kuweka mazingira kwa wasichana kupata ujuzi wa teknolojia ya mawasiliano. 

Sauti
3'46"
UNICEF/Tremeau

Msitu wa Bugoma ni uhai kwa maisha yetu-Uganda

Misitu ya asili kote duniani, kwa miaka mingi imekuwa sehemu muhimu ya maisha ya binadamu. Mathalani nchini Uganda, msitu wa Bugoma si tu unatunza historia ya asili ya watu wa eneo hilo, bali pia, wakazi wa eneo hilo wanasema vyanzo vingi vya maji ya mito ya eneo hilo ni katika mstu huo ambao pia unawapa dawa za asili za mitishamba zinazotumika katika tiba ya asili ya kiafrika. Katika makala ifuatayo, John Kibego, mwandishi wetu wa Uganda anapeperusha hewani maoni ya  wenyeji wa msitu wa Bugoma kuhusu tishio la kuchafuliwa kwa kiasi kukubwa cha msitu huo wa akiba.

Sauti
3'4"
© UNHCR/Rocco Nuri

Watoto wakimbizi wahusishwa katika kupambana na COVID-19 Uganda

Mlipuko wa COVID-19 duniani umetia mashakani karibu malengo yote ya Maendeleo endelevu au SDGs baada ya kukwamisha elimu, usafiri na uchumi miongoni mwa mengine. Hali imekuwa mbaya zaidi miongoni mwa wakimbizi kutokana na changamoto za uhaba wa rasilimali ambazo kawaida huwakumba hasa idadi yao inapoongezeka  bila kutarajiwa. Hata hivyo, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR na wadau wake nchini Uganda wameanzisha ushirikishwaji wa watoto wakimbizi katika juhudi za kupambana na COVID-19 wakati huu ambapo takribani wakimbizi mia moja wameambukizwa.&nbs

Sauti
3'24"
UN/Ahimidiwe Olotu

Ikiwa una ndoto lakini unahisi unaelekea kukata tamaa kutokana na vikwazo, sikiliza hii.

Katika maisha yake yote hadi sasa, kijana Narsent Charles Meena, ameishi na ndoto yake ya kusomea urubani ili siku moja aweze kuendesha ndege. Ndoto yake hiyo tayari imemfikisha katika kufanya kazi katika viwanja vya ndege na hata kufanya kazi katika ndege. Jambo moja ambalo hata hivyo hajalifikia ni kuendesha ndege. Je, karanga za shilingi 500 anazoziuza zitamwezesha kupata shilingi milioni 150 za Tanzania sawa na takribani dola elfu 65 ili aweze kusomea urubani? Ahimidiwe Olotu wa Kituo cha habari za Umoja wa Mataifa amemhoji kijana huyu.

 

Sauti
3'29"