Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

World Bank/Curt Carnemark

Tanzania tumeshinda tuzo na utalii umerejea– TTB

Wakati janga la ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19 likiendelea kusababisha zahma kwingineko duniani na hata kukwamisha shughuli za kiuchumi na kijamii, nchini Tanzania hali ni tofauti, utalii umerejea na tuzo juu ya kimataifa, kulikoni?  Stella Vuzo wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa, UNIC jijini Dar es salaam, Tanzania amemhoji Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania, TTB, Devotha Mdachi.

 

Sauti
6'1"
© UNICEF/Karin Schermbrucke

Kampeni za nyumba kwa nyumba, eneo kwa eneo zatokomeza Polio Afrika

Polio! Polio! Polio! Ugonjwa uliokuwa ukilemaza watoto 75,000 kila mwaka wakati wa miaka ya 1990 katika nchi za Afrika wanachama wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa kanda ya Afrika. Mataifa hayo ni 47 barani Afrika isipokuwa Somalia, Sudan, Eritrea, Misri, Libya na Tunisia. Gonjwa hilo halina tiba bali lina kinga ambayo ni chanjo, kinga ambayo viongozi kuanzia wa kaya hadi kimataifa walisimamia kidete kuhakikisha inamfikia kila mtoto barani Afrika na tarehe 25 mwezi huu wa Agosti, ukanda huo umetangazwa kuwa hakuna tena Polio! Nini kimefanyika?

Sauti
3'58"
UN/Imani Nsamila

Mafunzo tuliyoyapata yatasaidia kulifikia lengo namba 5 la SDGs -Wasichana Tanzania

Wasichana 28 nchini Tanzania wamenufaika na mafunzo ya upigaji picha yaliyofanywa na mpiga picha maarufu nchini humo, Imani Nsamila, kwa kushirikiana na shirika la Ladies Joint Forum na Kikoi innovative media. Ni mafunzo yanayolenga kuleta usawa wa kijinsia katika tasnia hiyo inayozidi kukua katika zama hizi za ukuaji wa teknolojia ya dijitali.  Kupitia makala hii, baadhi ya wasichana hao wanaeleza namna walivyonufaika na mafunzo hayo na watakavyoyatumia katika maisha yao. 

Sauti
3'44"
UN Women /Aidah Nanyonjo

Wanawake waimarisha ushiriki kwenye siasa za Uganda

Kufuatia juhudi za shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake, UN Women za kuwezesha wanawake, kupitia wadau mbalimbali duniani kote, kumekuwa na hatua chanya katika nchi kadhaa zikiwemo zile za Afrika Mashariki.

Kwa sasa ni bayana kwamba wanawake wanajitokeza kugombea nafasi mbalimbali za kisiasa na mara nyingine kuwashinda wanaume hali hiyo ikiwa ni tofauti na zamani ambapo ulikuwa ni mwiko kwa mwanamke kusimama mbele hadharani na kuongea.

Sauti
3'47"
World Bank/Maria Fleischmann

Tumenufaika sana na mafunzo ya lishe endelevu-Morogoro

Wanawake 40 na wanaume 21 wamenufaika na mafunzo kuhusu lishe endelevu, mafunzo ambayo yamefanyika katika eneo la Mvomero, Turiani Morogoro Tanzania kwa usimamizi wa shirika la Save the Children. John Kabambala wa redio washirika Kids Time FM amewahoji baadhi yao wakieleza mafunzo yalivyowasaidia na kuwa watayatumia kwenda kuelimisha wengine katika maeneo yao. 

Sauti
3'43"
UN/Imani Nsamila

Kuna pengo kubwa kati ya wanaume na wanawake kwenye tasnia ya upigaji picha Tanzania -Nsamila

Nchini Tanzania, mpiga picha maarufu, Imani Nsamila kwa kushirikiana na shirika la Ladies Joint Forum na Kikoi innovative media, kwa siku tano wamewapa mafunzo ya upigaji picha wasichana 28 ikiwa ni moja ya harakati za kuyafikia malengo Umoja wa Mataifa ya maendeleo endelevu, SDGs, kama vile lengo namba 5 linalolenga ulimwengu kuwa na usawa wa kijinsia kufikia mwaka 2030. Ahimidiwe Olotu wa Kituo cha habari cha  Umoja wa Mataifa UNIC Dar es Salaam amemhoji Imani Nsamila ambaye anaanza kwa kueleza alisukumwa na nini kuanza na kundi hili? 

 

Sauti
3'24"
UN/ John Kibego

COVID-19 yamuondoa mwimbaji jukwaani na kumrejesha kwenye useremala

COVID-19 imekuwa na madhara makubwa kwa vijana kote duniani kuanzia kipato hadi ustawi wa kijamii kutokana na wengi wao kupoteza ajira.

Hali hii ambayo imedumu kwa miezi nane sasa katika baadhi ya nchi imewalazimu vijana kuwa wabunifu zaidi na kutafuta njia mbadala za kipato ili kuepuka kuepuka maisha magumu.

Nchini Uganda, kijana mwimbaji Gerald Mutabaazi  aliamua kukimbilia msituni na kuanza sanaa ya kutengeneza vifaa vya upishi ili mikono ya wanafamilia yake iende kinywani.

Sauti
3'44"
UN/Rose Nyabhate

Safari ya wasichana na wanawake kuingia kwenye kiwanda cha uchekeshaji Kenya, haikuwa rahisi-Nyabheta 

Taaluma ya ugizaji inaendelea kubadilika kila uchao katika nyakati ambazo teknolojia ya mawasiliano inazidi kukua.  Nchini Kenya kwa sasa, tasnia ya uigizaji na uchekeshaji imeajiri vijana wengi wa kiume na wa kike ingawa safari ya kundi moja kati ya hayo mawili haikuwa rahisi. Je wanawake wamechukua nafasi gani katika taaluma ya uigizaji na uchekeshaji kwa sasa? Jason Nyakundi amezungumza na mchekeshaji wa miaka mingi wa vipindi vya televisheni nchini Kenya Rose Nyabhate  kutaka kujua safari yake imekuwa ya aina gani katika tasnia hii. 

Sauti
3'36"
UN News/ John Kibego

Kwa sasa nimewaambia wakimbizi wenzangu tusishikane mikono, tusitembeleane- Acces Bazibuha  

Sasa ni makala ambapo tunafuatilia hali ilivyo na mikakati inayowekwa na wadau mbalimbali yakiwemo mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la kuhudumia wakimbizi UNHCR, la afya WHO na wizara ya afya ya nchini hiyo kuzuia kuenea kwa COVID-19 kufuatia mlipuko wake katika makazi ya wakimbizi ya Kyangwali na kusababisha kifo cha mkimbizi mmoja hapo tarehe nane Agosti mwaka huu. Moja ya hatua ilikuwa ni kuzuia watu kutembea huku na kule, na pia kufuatilia watu waliokutana na mkimbizi aliyeambukizwa. 

Sauti
54"
© UNICEF/Zahara Abdul

Maziwa ya ng'ombe yana protini isiyoweza kumeng'enywa kwenye tumbo la mtoto mwenye umri wa chini ya miezi 6 - Mtaalamu

Ni mwaka mmoja tangu mradi wa mafunzo kuhusu lishe endelevu ulipoanzishwa mkoani Morogoro kwa ufadhili wa shirika la Save the Children na shirika la Marekani la msaada wa kimataifa USAID. Sehemu ya mradi huo ni kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa mtoto kunyonya maziwa halisi ya mama angalau kwa miezi sita ya kwanza. Je, wanuafaika wa mradi huo wanasemaje? Wameelimika kwa kiasi gani tangu mradi huo kuanzishwa mwezi Agosti mwaka jana 2019? John Kabambala wa redio washirika Kids Time FM amezungumza nao na kuandaa makala hii. 

Sauti
3'25"