Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

UN Women /Aidah Nanyonjo

Mimi kama mbunge ni wajibu wangu kuielimisha jamii jinsi ya kujikinga na COVID-19-Mbunge David Karubanga wa Uganda

Leo ni siku ya mabunge duniani ambapo mchango muhimu wa mabunge na wabunge unatambuliwa katika kuwawakilisha wananchi na kupaza sauti zao ili serikali imweke mwanajamii katika katika vipaumbele vyake inapoweka mipango ya nchi. Katika zama hizi za COVID-19, mabunge na taasisi nyingine za serikali nazo zimelazimika kwa kiasi fulani kufuata utaratibu mpya kujikinga na virusi ikiwemo kuweka umbali kati ya mtu na mtu na hata wakati mwingine kulazimika kufanya kazi nje ya majengo ya bunge kama ilivyo kawaida.

Sauti
3'39"
UNEP/Cyril Villemain

Havillah Smart Enviros si tu tunaokoa mazingira, bali bila tunasaidia kuzalisha ajira Kenya

Huku mirundiko ya taka ikiendelea kushuhudiwa katika miji mingi hususan kwenye nchi zinazoendelea, katika miaka ya hivi karibuni baadhi ya wakazi wa miji hii wamekuwa wakibuni njia za kujipatia kipato kutokana na taka hizi, hatua ambazo kwa upande mwingine  zimechangia katika kuboreka mazingira ya mijini. Mjini Nairobi, kampuni inayofahamika kama Havillah Smart Enviros imejikita katika kukusanya taka ngumu, kuziandaa na kuzirudisha katika viwanda ili kutengenezwa tena bidhaa. Jason Nyakundi amezungumza na mwanzilishi  ya kampuni hiyo Samueli Maina Wangoi.

Sauti
4'52"
IMO

Tumejisikia fahari kutokana na hatua ya kuhamasisha kazi yetu itambulike kama kazi ya muhimu-Mabaharia 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia ujumbe wake kuhusu siku ya baharia inayoadhimishwa hii leo kama ilivyo ada ya kila tarehe 25 ya mwezi Juni, ametoa wito kwa mataifa, serikali na jamii kwa ujumla kuwapa heshima wanayositahili mabaharia kwani kwa muda mrefu wamekuwa wakifanya kazi ya kishujaa ambayo haikuwa imepewa uzito wa kutosha. Bwana Guterres amesema nyakati hizi za COVID-19 zimeonesha wazi ni kwa namna gani kazi ya ubaharia ni ya muhimu kwa mabaharia waliendelea kuchapa kazi wakati wote pamoja na changamoto mbalimbali. Je, mabahari wanaipokeaje hatua hii?

Sauti
3'47"
WFP/Henry Bongyereirwe

Tumaini katika biashara ya mkimbizi kati ya changamoto za COVID-19, Uganda

Licha ya changamoto za biashara kudorora kutokana na vikwazo vya kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona au COVID-19, wanawake wakimbizi nchini Uganda wanajitahidi kuendelea kujikimu wakiwa na matumaini siku moja mambo yatarejea kuwa kama kawaida. Basi ungana na John Kibego aliyetembelea jamii ya wakimbizi na kuzungumuza na mkimbizi mjasiriamali kutoka Rwanda.

 

Makala hii imetayarishwa na John Kibego

Sauti
3'27"
WFP/Henry Bongyereirwe

Tumaini katika biashara ya mkimbizi kati ya changamoto za COVID-19, Uganda

Licha ya changamoto za biashara kudorora kutokana na vikwazo vya kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona au COVID-19, wanawake wakimbizi nchini Uganda wanajitahidi kuendelea kujikimu wakiwa na matumaini siku moja mambo yatarejea kuwa kama kawaida. Basi ungana na John Kibego aliyetembelea jamii ya wakimbizi na kuzungumuza na mkimbizi mjasiriamali kutoka Rwanda.

Sauti
3'27"
© Julius Mwelu/ UN-Habitat

Jamii haikubali kifo, mume anapofariki dunia, huamini mke amemuua- Christine

Hii leo ulimwengu unaadhimisha siku ya kimataifa ya wajane ambao mara nyingi wanapobakia wenyewe pindi wenza wao wanapofariki dunia ni kutaabika kiuchumi na kijamii. Mathalani taabu katika kulea watoto na changamoto nyingine za kifamilia. Katika kumulika changamoto hizo, mwandishi wetu wa Nairobi, Kenya,  Jason Nyakundi amezungumza na Christine Iganza kutoka Vihiga Magharibi mwa Kenya ambaye alibaki  mjane  mwaka 2008 na watoto 4 akiwemo mmoja mwenye umri wa wiki tatu. Christine anaanza kwa kuelezea maisha yalivyobadilika.
 
TAGS: , Wajane

 

Sauti
5'21"
UN News/Video capture

COVID-19 imeongeza ugumu katika changamoto za awali za watu wenye ualbino lakini na mwanga upo

Katika kipindi cha takribani miaka kumi nyuma kufikia mwaka 2015 nchini Tanzania kulisheheni matukio mengi ya kutisha yaliyohusisha mauaji au kujeruhiwa kwa kukatwa viungo watu wenye ualbino kutokana na imani za kishirikina. Wadau wa masuala ya haki za watu wenye ualbino wanasema kama si mlipuko wa COVID-19 kuwaongezea matatizo katika changamoto za muda wote kama vile uoni hafifu na matatizo ya ngozi, watu wenye ualbino walikuwa wameanza kuuona unafuu wa maisha kutokana na kupungua kwa matukio ya mauaji dhidi yao.

Sauti
4'12"
UN/ Jason Nyakundi

Nilimchora Ronaldihno na kufanikiwa kumkabidhi picha yake - Art Dehnow Mgenge

Kama ilivyo kwa wasanii wengine wakiwemo wanamuziki  au wachekeshaji pia wasanii wa kuchora nao wako na nafasi yao katika jamii. Akitumia penseli yake, kijana mmoja nchini Kenya, amewachora watu mashuhuri na hata kuwafikia baadhi yao na kuwakabidhi picha hizo na hivyo kwa kiasi kuendesha maisha yake kwanjia hiyo. Na zaidi ya hayo msanii huyo sasa ndoto yake ni kukusanya vijana wengine na kuwafundisha stadi hiyo. Mwandishi wa Nairobi Kenya Jason Nyakundi alimtembelea msanii huyo na kuzungumza naye.

Sauti
2'7"