Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNDP yapiga jeki juhudi za wakulima wa pilipili Tanzania

UNDP yapiga jeki juhudi za wakulima wa pilipili Tanzania

Pakua

Nchini Tanzania harakati za kuondokana na umaskini zinaendelea kushika kasi mashinani zikipigiwa chepuo na Umoja wa Mataifa. Miongoni mwa hatua hizo ni kilimo cha kisasa cha mboga mboga na matunda kinachoendeshwa na wanawake kupitia chama cha wakulima wa mboga na matunda nchini Tanzania, TAHA. TAHA imepatiwa msaada na shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP nchini Tanzania na sasa kupitia vikundi mbalimbali, wakulima wanalima mazao ambayo yanakidhi vigezo vya kuuzwa nje ya nchi. Hivi karibuni Sawiche Wamunza, mtaalamu wa mawasiliano UNDP Tanzania alitembelea shamba la mfano la kilimo cha pilipili kwa ajili ya mauzo nje ya nchi, Habanero model farm for Commercial Habanero production for Export market na amezungumza na mmoja wa wakulima Betty Gadson Mrema.

Audio Credit
Grace Kaneiya/ Sawiche Wamunza
Sauti
5'38"
Photo Credit
UNDP Tanzania/Sawiche Wamunza